UHALIFU WA SIRAHA:-Majambazi yamuua Sista Ubungo Dar es Salaam kisha Kutokomea na Mkoba wake. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 23, 2014

UHALIFU WA SIRAHA:-Majambazi yamuua Sista Ubungo Dar es Salaam kisha Kutokomea na Mkoba wake.

Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi leo June 23, 2014,tukio lililotokea eneo la Ubungo-Darajani karibu na River Side Jijini Dar es Salaam.


Hali ya hewa imechafuka kwa wakazi wa eneo la Ubungo-Darajani karibu na River Side Jijini Dar es Salaam ,baada ya majambazi kumuua Sista wa Parokia ya Makoka-Mwisho aliyefahamika kwa jina moja la Kapuli na kisha kumjeruhi dereva wa gari na kutokomea na mkoba wa marehemu kusikojulikana.

Tukio hilo la kinyama limetokea majira ya saa 7 na nusu leo June 23,3014,mchana wakati sista huyo aliyekuwa na dereva wakitokea benki kufika eneo hilo kwa lengo la kununua mahitaji muhimu.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni dereva wa gari aliyefahamika kwa jina la Mark Patrick Mwarabu alisema kuwa marehemu alishangaa kuona amezungukwa na watu watatu waliokuwa wameshuka kwenye pikipiki aina ya Boxer na kumfuata kisha kumpiga risasi kadhaa.

Aliongeza kuwa, marehemu alikuwa ameenda kulipia pesa kwa ajili ya kununua mchele kwenye duka moja la nafaka kabla ya kuvamiwa na majambazi hao waliompiga risasi na kutokomea na mkoba wake huku wakimpiga risasi dereva huyo kidoleni.

(HABARI/PICHA: Deogratius Mongela / GPL).


Kidole cha dereva kilichokatwa kwa risasi.

Ganda la risasi likiwa eneo hilo la tukio.

Gari alilokuja nalo marehemu Sista Kapuli.

...Dereva akiwasiliana na jamaa zake baada ya kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa.

Gari lenye namba za usajili T 213 CJZ alilokuja nalo Marehemu.

Mwili wa sista ukiingizwa kwenye gari la polisi.


Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakichukua matukio eneo hilo la eneo la Ubungo-Darajani karibu na River Side Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad