MBUNGE AUAGA UKAPERA:-Tazama Yaliyojiri wakati Mbunge JOSHUA NASSARI alipofunga ndoa na Bi.ANNA NNKO, USA RIVER jijini ARUSHA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 09, 2014

MBUNGE AUAGA UKAPERA:-Tazama Yaliyojiri wakati Mbunge JOSHUA NASSARI alipofunga ndoa na Bi.ANNA NNKO, USA RIVER jijini ARUSHA.


"Mmetuona "ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa…
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Samwel Nassari amefunga ndoa na Anande Nnko kwenye Kanisa la Pentekoste lililopo Kilinga, Arumeru jijini Arusha ikifuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hoteli ya Ngurdoto…

Sherehe hiyo ilianza mishale ya saa 7:00 mchana siku ya June 07,2014 ambapo watu wote walialikwa wakiwemo ndugu, marafiki, jamaa na wananchi wote wa Arumeru Mashariki ambao wamepiga ‘mpunga’ wa kutosha na vinywaji hadi kila mtu akaondoka akisema ‘Nassari ameacha historia’.


Gavana wa kwanza wa Tanzania Mzee Edwin Mtei na Mama Mtei pia walikuwa katika inada hiyo.


Wazazi wa Maharusi ,Joshua Nassari na Bi Anande Nnko.


Bw na Bi Joshua Nassari na wakiweka Sadaka zao katika kapu la sadaka.


Maharusi ,wakapata nafasi ya kusalimiana na Mzee Edwin Mtei.


Ibada ya ndoa ikawa imefika tamati na maharusi wakatoka kanisani tayari kwa msafara wa magari kuelekea uwanjani.



Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiwa mbele ya zawadi yao ya
Ng'ombe ilitolewa na waumini wa Kanisa la Kilinga ambako ibada ya ndoa
ilifanyika,kanisa linaloongozwa na Mchungaji Babu.


Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiteta jambo .


Baba Mzazi wa Joshua Nassari,Mzee Samwel Nassari akimpongeza mwanae kwa hatua hiyo.


Mamsapu akianza majukumu ya kuhakikisha Mzee anakuwa nadhifu kila wakati.



Bi Harusi Anande Nnko akiwa katika gari tayari kuelekea katika viwanja vya Usa-River Academy.


Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari na ,Anande Nnko
wakiwa ndani ya gari muda mfupi baada ya kufunga ndoa katika kanisa la
Kilinga wilayani Arumeru tayari kwa kuelekea viwanja vya  Usa-River
Academy.



Msafara ukaanza safari ya kuelekea barabara kuu ya Moshi/Arusha ukitokea kanisani Kilinga.


Baadae maharusi wakabadili gari ili waweze kuonekana vyema na wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki.


Maharusi wakiwa katika gari la wazi huku wakipunga mikono kwa watu waliokuwa barabarani.



Kila sehemu msafara wa magari ya maharusi ulipopita ,wakazi wa maeneo hayo walionesha furaha zao .

Barabarani kulijaa watu wakimshangilia Mbune wao akijinyakulia Jiko.

......''' Kama kawaida Jasiri haachi asili na muacha asili ni hasidi na hana akili..''........


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad