Kwa pamoja wanamuziki nguli wa dansi
Bongo, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’
wakitumbuiza.
|
Wakati
wakitimiza miaka 10 gerezani tangu walipohukumiwa Juni 25, 2004, mwanamuziki
nguli wa dansi Bongo, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii
Kocha’ wametoa watu machozi kwa mara nyingine.
Wakitumbuiza
na kukumbushia enzi zao mwishoni wiki iliyopita kwenye sherehe ya siku ya
magereza nchini iliyofanyika katika Chuo cha Maofisa Magereza, Ukonga, Dar,
wanamuziki hao walitoa burudani ya kihistoria mbele ya mgeni rasmi, Waziri wa
Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, kamishna wa magereza nchini, John Minja na
mkuu wa magereza wa Namibia, Raphael Tuhafeni Hamunyela.
Mwanamuziki nguli wa dansi Bongo, Nguza Viking
‘Babu Seya’ akilirindimisha gitaa la solo.
|
BABU
SEYA, PAPII WAHUZUNISHA.
Wanamuziki hao ambao wanatumikia kifugo cha maisha, waliimba wimbo ambao uliwahuzunisha wengi kutokana na ujumbe uliomo katika mashairi hayo.
Sehemu ya
mashairi hayo ilisema: ’’Magereza si sehemu ya mateso bali ni sehemu ya
kujifunza na kurekebishwa, JK tusamehe, tumejirekebisha, mgeni rasmi (Chikawe)
tuombee kwa rais atupe uhuru wafungwa wote tumejifunza, hata Petro alimkana
Yesu mara tatu lakini alisamehewa sembuse sisi kwani ni kipi tulichokosa
sisi?’’
...Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ naye akifanya
yake...
|
MIAKA 10
GEREZANI.
Juni 25, 2004 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, iliwatia hatiani Babu Seya na wanaye Papii, Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya ubakaji na unajisi wa watoto.
Januari 27,
2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa
yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote
waliyokuwa wameshitakiwa nayo.
Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias
Chikawe aliyehudhuria maadhimisho ya siku ya Magereza.
|
Jaji
Mstaafu, Mihayo, Septemba 15, 2011 aliwahi kunukuliwa akikanusha uvumi
ulioenea kuwa, kiongozi mmoja mkubwa wa serikali aliwashinikiza majaji ili
watoe hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na wanaye.
“Hakika si
kweli…Niliupitia mwenendo wa kesi hiyo na kubaini kwamba kilichokuwa kinasemwa
mitaani kilikuwa ni uvumi usiokuwa na chembe ya ukweli,” alisema Jaji Mihayo
alipokuwa akizindua rasmi Ripoti ya Ufuatiliaji wa Vyombo vya Habari vya
Magazeti (Julai 2010-Juni 2011) ya Baraza la Habari la Tanzania (MCT) jijini
Dar es Salaam.
...Askari wakipiga gwaride kama sehemu ya
maadhimisho hayo.
|
Alisema
aliusoma kwa kina mwenendo wa kesi ya kulawiti dhidi ya Babu Seya na wanawe
kama ulivyoandaliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kabla ya kutoa hukumu
ya mwisho.
Alisema kwa kuwa mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kuamua kuhusiana na shauri hilo, ilipokea ukweli wa mwanzo wa shauri hilo na ikauwasilisha Mahakama Kuu.
Alisema
wakati akizisoma nyaraka na mwenendo wa kesi kutoka katika mahakama hiyo ya
chini (Mahakama ya Kisutu), aligundua kwamba kilichokuwa kikisemwa na watu
mitaani ulikuwa ni uvumi tu.
Jaji Mihayo alisema alitenga muda wa kuongea na watoto waliodaiwa kubakwa na Babu Seya na wanaye na akagundua kwamba watoto hao walikuwa wamelawitiwa na kwamba tendo hilo lilikuwa limefanywa kwa kipindi cha miezi kadhaa.
Alisema
aliwasikiliza watoto hao na akapata picha kamili ya kilichoendelea katika
matukio hayo na pia aligundua kwamba wazazi wa watoto hao hawakuwa wanajua
mwenendo wa watoto wao.
Alifafanua kwamba baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vikitoa ripoti isiyo sahihi ya kesi hiyo na akasema kwamba kama waandishi wangefanya uandishi wa kiuchunguzi, wangeweza kupata ukweli wa tukio hilo.
Hata hivyo,
baada ya kesi yao kusimamiwa na wakili Mabere Marando, jopo la majaji
watatu wa mahakama ya rufaa lililokuwa na majaji Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk
na Salum Massati katika hukumu yao iliyotolewa Februari 2010, mahakama hiyo
iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanaye, Papii huku
ikiwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Mbangu, na Francis.
Oktoba 30,
mwaka jana, Mahakama ya Rufaa iliyoketi chini ya jopo la majaji watatu,
likiongozwa na Nathalia Kimaro, akisaidiana na Mbarouk Mbarouk na Salum Masati
walisikiliza hoja za pande zote kuhusu ombi la kufanyika marejeo ya uamuzi wa
awali wa mahakama hiyo.
Mahakama
hiyo baada ya kufanya mapitio iliendelea kuwaona warufani hao wawili kuwa na
hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu yao.
Juu ya vilio
vya wanamuziki hao kuomba rais kuwaachia huru, Marando alisema rais ni mtu
mkubwa hivyo anaweza kusikiliza vilio vyao.
Ilidaiwa
kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo hivyo kati ya Aprili na Oktoba 2003 maeneo
ya Sinza Kwaremmy, Dar Es Salaam.
Stori:- Haruni Sanchawa, Gabriel Ng'osha na Makongoro Oging’
No comments:
Post a Comment