Baada ya
ajali hiyo.....
|
Inavyoonekana
kwa nyuma
|
Lori la Mizigo aina ya Scania
lililogongwa kwa nyuma.
|
....Sehemu
ambayo gari hilo dogo liliingia nyuma ya Lori hilo.....
|
Ajali mbaya
iliyohusisha gari dogo aina ya Land Rover Freelander lenye namba T368 CVK na
roli la mizigo aina ya Scania lenye namba T346 BRF imetokea usiku wa juzi (June 22,2014)
katika eneo la Lugemba, kilomita kadhaa kabla ya kufika mji wa Mafinga.
Taarifa za awali zinaonesha kwamba dereva wa gari hilo jina lake bado
halijapatikana alifariki papohapo baada ya gari yake kuingia nyuma ya roli hilo
lililokuwa limepaki kandakando ya barabara ya Mafinga Dar es Salaam, akiwa
katika mwendo mkali.
Mwanafunzi
wa kike wa Chuo Kikuu cha Tumaini aliyekuwemo katika gari hilo amenusurika kufa;
binti huyo ambaye pia jina lake halikupatikana amelazwa katika hospitali ya
wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na kukatika mkono.
Mashuhuda wa
tukio hilo wamesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 3 usiku. Na baada ya ajali
hiyo wasamalia wema waliukumbiza mwili wa marehemu na majeruhi katika hospitali
ya wilaya ya Mufindi.
Jeshi la
Polisi limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na taarifa za awali zinaonesha
dereva wa gari hilo alikuwa amelewa wakati akiendesha gari hilo.
Habari/Picha Na:-FRANCIS GODWIN-IRINGA.
No comments:
Post a Comment