...Daladala hiyo
inavyoonekana mara baada ya ajali.....
|
.......Askari wa usalama akichukua
maelezo eneo la tukio........
|
.......Wananchi wakiwa eneo la
tukio......
|
.....Baadhi ya miili ikiwa kwenye
gari Hospitali ya Lugalo......
|
....Daktari akiendelea kutoa
huduma ya kwanza ndani ya gari la wagonjwa.....
|
Madaktari wa Hospitali ya
Lugalo wakiendelea kuwahudumia majeruhi.
|
Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Lugalo, Brigedia Jeneral, Josia Mekere.
|
...Baadhi ya
maaskari na wananchi waliokuwa wakitoa huduma ya kwanza eneo la tukio. ...
|
........Mzee aliyefiwa na mwanae
akilia kwa uchungu..............
|
.......Ndugu wakilia kwa uchungu
baada ya kutambua miili ya ndugu zao....
|
...eneo la ajali
linavyoonekana mchana wa Leo June 21, 2014.....
|
Kushoto ni gari ndogo aina ya
Range Rover ambayo iligongwa na Daladala (kulia) iliyosababisha ajali hiyo leo June
21, 2014,mchana.
|
Watu sita wamepoteza maisha
na wengine kumi na mbili wakijeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea eneo la
Makongo barabara ya Bagamoyo jijini
Dar–es–salaam,ikiyahusisha magari manne, mawili kati ya hayo yakiwa ni ya abiria
maarufu kama Daladala,zifanyazo safari zake kati ya Ubungo,Mwenge,Makumbusho na
Tegeta.
Vilio na simanzai vilitawala
kwenye maeneo yanayozunguka hosipitali kuu ya jeshi la wanachi wa Tanzania
(JWTZ) Lugalo jijini Dar–es–salaam,ambapo mashuhuda wa ajali hiyo wanadai
kuwa,dereva aliyekuwa akitokea tegeta kwenda mwenge alikuwa katika mwendo wa
kasi ya ajabu.
Mganga mkuu wa hosipitali ya
jeshi lugalo iliyopokea majeruhi na maiti hao,Brigedia Jenerali Dkt Makere
Josiah,amethibitisha kupokea majeruhi kumi na wawili na maiti sita,huku wengine
hali zao zikiwa ni mbaya na kukimbizwa kwenye hosipitali ya taifa ya rufaa
Muhimbili kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment