KUNYWA SUMU/KUJINYONGA-NGARA:-Afa kwa kujinyonga kwa kutumia kipande cha kitenge …..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 12, 2014

KUNYWA SUMU/KUJINYONGA-NGARA:-Afa kwa kujinyonga kwa kutumia kipande cha kitenge …..’’


Mwanamke mmoja  mkazi wa kitongoji cha Ruhembe,Kata ya  Mkurukuzo wilayani Ngara  mkoani  Kagera, amekutwa amejinyonga nyumbani  kwa Mama yake mzazi  alipokuwa ameenda kumtembelea kitongoji cha Katenga..Picha Na:-Maktaba yetu.

Afisa mtendaji  wa kijiji cha Mkurukulazo Bi  Lidia  Mathias  amemtaja  mwanamke huyo aliyejinyonga  kuwa  ni  Jilian  Philimoni mwenye umri wa miaka 52.

Naye  Diwani wa kata ya  Murukulazo Bw  Mukiza Byamungu amesema  tukio hilo limetokea June 10, 2014,  saa 8 mchana ambapo  alijinyonga kwa kutumia kipande cha kitenge   na kwamba marehemu hakuacha ujumbe wowote  juu ya sababu za kujinyonga kwake.

Jeshi la Polisi wilayani Ngara limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba linaendelea na uchunguzi .
 
Habari Na:-Radio kwizera FM-Ngara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad