|
Timu ya Taifa ya Ghana Leo June
21, 2014, huko Brazil wameilazimisha sare ya 2-2 Timu ya Ujerumani kwenye Mechi yao ya Pili ya Kundi G la Fainali
za Kombe la Dunia 2014.
Kwenye Mechi ya Kwanza, Ghana
walifungwa 2-1 na USA na Ujerumani kuitwanga Portugal Bao 4-0.
Magoli ya Timu hizo
yamefungwa na Mario Gotze dakika ya 51 na Klose dakika ya 71' huku Ghana goli
zikifungwa na A.Ayew (54'),Gyan (63')
|
|
Mechi nyingine ya Kundi G
itachezwa Jumapili June 22,2014 kati ya USA/Marekani na Portugal. |
|
Timu ya Taifa ya Argentina
imefuzu hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia 2014, baada ya kuilaza Iran bao 1-0
kwa mbinde jioni ya June 21, 2014,katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mineirao
mjini Belo Horizonte, Brazil.
Shukrani kwake Nahodha wa
timu hiyo, Lionel Messi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya kwanza ya muda wa
nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida za mchezo huo, akifumua shuti kutoka
umbali wa mita 25.
Argentina sasa inatimiza
pointi sita baada ya mechi mbili na kusonga mbele, ikiwaachia Iran, Nigeria na
Bosnia kibarua cha kuwania nafasi ya pili ya kufuzu kutoka kundi hilo.
Iran waliibana haswa
Argentina katika mchezo wa leo na ilibaki kidogo tu wafanikiwe kupata sare,
sifa zimuendee kipa wao Haghighi aliyeokoa michomo mingi ya hatari.
|
|
Lionel Messi akishangilia
baada ya kuifungia bao pekee Argentina dhidi ya Iran leo June 21, 2014,waliposhinda
bao 1-0.
|
KOMBE LA DUNIA 2014-RATIBA/MATOKEO.
JUMAMOSI, JUNI 21, 2014
|
SAA
|
MECHI
|
KUNDI
|
UWANJA
|
1900
|
Argentina 1 Iran 0
|
F
|
Estadio Mineirão
|
2200
|
Germany v Ghana
|
G
|
Estadio Castelão
|
0100
|
Nigeria v Bosnia-Herzegovina
|
F
|
Arena Pantanal
|
JUMAPILI, JUNI 22, 2014
|
SAA
|
MECHI
|
KUNDI
|
UWANJA
|
1900
|
Belgium v Russia
|
H
|
Estadio do Maracanã
|
2200
|
South Korea v Algeria
|
H
|
Estadio Beira-Rio
|
0100
|
United States v Portugal
|
G
|
Arena Amazonia
|
JUMATATU, JUNI 23, 2014
|
SAA
|
MECHI
|
KUNDI
|
UWANJA
|
1900
|
Australia v Spain
|
B
|
Arena da Baixada
|
1900
|
Netherlands v Chile
|
B
|
Arena Corinthians
|
2300
|
Croatia v Mexico
|
A
|
Arena Pernambuco
|
2300
|
Cameroon v Brazil
|
A
|
Nacional |
|
Argentina wamebakisha Mechi
moja na watacheza na Nigeria hapo Jumatano June 25, 2014.
|
As It Stands Tables FIFA World Cup 2014.
No comments:
Post a Comment