KOMBE LA DUNIA 2014:-Tamaza Yaliyojiri wakati Costa Rica,Italia na Ivory Coast wakipata ushindi wao wa kwanza katika Fainali za Kombe la Dunia June 14,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 15, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Tamaza Yaliyojiri wakati Costa Rica,Italia na Ivory Coast wakipata ushindi wao wa kwanza katika Fainali za Kombe la Dunia June 14,2014.

Luis Suarez  hakuweza kuangalia mpira baada ya timu yake ya Uruguay kupigwa mabao 3-1 dhidi ya Costa Rica kwenye mchezo wa ufunguzi wa kundi D na Ili kufuzu, Uruguay wana kazi kubwa hapo Alhamisi kuifunga England ambayo nayo imefungwa 2-1 na Uingereza.

Suarez alijawa na mawazo kutokana na kupigo wakati wa mchezo huo huko Fortaleza ndani ya Estadio CastelĆ£o, kwenye Mechi ya Kwanza ya Kundi D, Costa Rica walitandaza Soka safi na kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Uruguay Bao 3-1.

Ushindi huu umekuja kutokana na juhudi za Mchezaji wa Arsenal, Joel Campbell, ambae alifunga Bao moja na kutengeneza Bao jingine…

Edinson Cavani alitangulia kuwapa Uruguay Bao kwa Penati na kuongoza 1-0 hadi Mapumziko.

Kipindi cha Pili Costa Rica walicharuka na kufunga Bao 2 ndani ya Dakika 3 kupitia Joel Campbell na Oscar Duarte huku Marcos Urena, alietokea Benchi, akipachika Bao la 3 kwenye Dakika ya 84.

Suarez na wenzake katika Benchi la Ufundi la Uruguay wakiwahamasisha wenzao kwa kupiga kelele baada ya wenzake kupoteza nafasi za kufunga walipofungwa 3-1 na Costa Rica.

Timu ya Taifa ya Uingereza June 14,2014, kimeanza vibaya Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil baada ya kupokea kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Italia usiku huu. Katika mechi hiyo ya kundi D wafungaji wa Italia walikuwa ni Marchisio 35, Balotelli 50 na Uingereza likafungwa na Sturridge 37.

Straika wa Italia, Mario Balotelli (kushoto) akiifungia timu yake bao la ushindi dhidi ya Uingereza June 14,2014, usiku.

Daniel Sturridge akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake ya Uingereza katika dakika ua 37 dhidi ya Italia na Italia kushinda 2-1.

Wachezaji wa Italia wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Claudio Marchisio (jezi namba 8 kulia).

Mshumbuliaji wa Ivory Coast, Gervinho (kushoto) akishangilia bao lake na Didier Drogba wakati pale Timu ya Taifa ya Ivory Coast imeanza vizuri michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kuizamisha Japan bao 2-1 kwenye mechi ya kundi C iliyopigwa leo (June 15, 2014) alfajiri. Mabao ya Ivory Coast yamewekwa kimiani na Gervinho dakika ya 66 na Wilfried Bony dakika 64 huku la Japan likifungwa na Honda 16.

Keisuke Honda akiifungia Japan bao lao dakika ya 16....


Wilfried Bony akiifungia Ivory Coast bao la kwanza katika dakika ya 64.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad