KIUMBE WA AJABU:-Tazama Picha za Mtoto wa Ajabu aliyezaliwa mkoani Njombeakiwa na Umbo linalofanana na Chura. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 18, 2014

KIUMBE WA AJABU:-Tazama Picha za Mtoto wa Ajabu aliyezaliwa mkoani Njombeakiwa na Umbo linalofanana na Chura.

Mtoto wa ajabu amezaliwa huko wilayani Makete mkoani Njombe usiku wa kuamkia tarehe 17,june 2014.

Ukimuona mtoto ngozi yake ni kama amevaa koti kubwa kushinda uwezo wa mwili wake akiongea na blog hii reporter Daima Kyando alisema mtoto huyo wa ajabu alikua na tumbo kubwa lililomeza viungo vingine vya mwili kama miguu,mikono,kiuno na shingo.

Akiendelea zaidi reporter huyo  alisema mama wa mtoto huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja alikua na afya nzuri na kuonesha kuwa mimba yake ilikua ya kawaida kwani alihudhuria clinic kama kawaida na hakupatikana na matatizo yoyote. 

Habari zaidi zinasema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa amekwisha fariki na alizaliwa kwa njia ya upasuaji,huku chanzo cha tatizo la mtoto huyo hakikuweza kufahamika mara moja mpaka tunaenda mtandaoni madaktari walikuw wakiendelea na uchunguzi. 

Mama wa mtoto huo hakuweza kuongea lolote zaidi alilia kwa uchungu kwani na yeye alishikwa na bumbuazi juu ya kilichotokea akihisi ni ndoto. 

Ukimuangalia zaidi mtoto huyo unaweza kugundua kuwa ana umbo la chura,eeeeh mungu heal the world. 
MTOTO HUYO HAKUAZALIWA MZIMA ALIZALIWA AKIWA AMEKUFA
R.I.P 
Picha na Hotnewstanzania.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad