AJALI BARABARA YA LUSAHUNGA-RUSUMO:-Lori kubwa la Mizigo latumbukia Shimoni eneo la ziroziro-Ngara,Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 11, 2014

AJALI BARABARA YA LUSAHUNGA-RUSUMO:-Lori kubwa la Mizigo latumbukia Shimoni eneo la ziroziro-Ngara,Kagera.

Ajali hii imetokea June 08,2014 saa 12 jioni makutano ya Barabara ya kwenda Rusumo-Benaco-Lusahunga ,eneo maarufu la ziroziro wilayani Ngara mkoani Kagera baada ya Lori hilo la Mizigo lililokuwa likisafiri kwenda Rwanda kufeli mfumo wa breki na kutumbukia katika shimo lililopo barabarani hali iliyoliyumbisha na kumshinda dereva kisha kuhama barabara na kutumbukia pembezoni kama picha inavyoonyesha.




Baada ya kuhama barabara huku ndiko Lori hilo lilikotumbukia pembezoni mwa barabara na hakuna Mtu aliyepoteza kifo au Kujeruhiwa.


Ajali hiyo ilisababisha Kontena kutoka na Lori kubaki peke yake kwa kichwa cha Lori kuinuka juu,Hapa ikionekana baada ya kulikwamua na kuliweka sawa.


Kutokana na Ubovu wa Barabara hiyo ya Lusahunga-Rusumo na wakati Mwingine Madereva kuendesha magari hayo wakiwa wamechoka kwa safari ndefu,toka June 08,2014 ,jumla ya malori 3 yameanguka katika barabra hiyo,Moja eneo la Machinjioni na kuuwa Dereva wake papo hapo na lingine likianguka eneo la mteremko wa Nyabungombe June 11,2014 na kusababisha Majeruhi.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad