ZIARA YA CCM-TABORA:-Picha za Mkutano wa Hadhara Mei 09,2014 Viwanja vya Sokoine –Ndugu Kinana akihutubia maelfu ya Wanaigunga. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, May 10, 2014

ZIARA YA CCM-TABORA:-Picha za Mkutano wa Hadhara Mei 09,2014 Viwanja vya Sokoine –Ndugu Kinana akihutubia maelfu ya Wanaigunga.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga , Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya siku kumi kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua na pia kuimarisha uhai wa chama mkoani Tabora.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Mnauye akizungumza kwenye mkutano huo

Maelfu ya wananchi wakinyoosha mikono kumshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara Mei 9, 2014, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga,mkoani Tabora.

Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora Elibariki Kingu, akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye mkutano huo wa Kinana auliofanyika, Mei 9, 2014 kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine wilayani humo.

Kinana akirudi hotelini kwa miguu baada ya mkutano, pembeni yake ni Nape.

KUIMARISHA UHAI WA CHAMA :-Kinana akizindua Ofisi ya CCM tawi la Igogo, Kata ya Nanga Igunga, mkoani Tabora,Mei 9, 2014.

 Kinana akizungumza baada ya kuzindua Ofisi hiyo ya CCM tawi la Igogo, Kata ya Nanga Igunga. Kulia kwake ni Nape.

Kinana akisalimia baadhi ya wazee baada ya kuzindua tawi hilo la Chama cha Mapinduzi-CCM.

Katibu mkuu CCM,Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Mihama, wilayani Igunga mkoani Tabora, Mei 9, 2014. Kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Igunga, Bw.Elibariki Kingu akisaidia kubeba tofali kumpa Katibu Mkuu Kinana.

Kinana akiwa na bango lenye ujumbe maridhawa, kumkaribisha Kinana, alipotembelea shamba la alizeti la Vijana wajasiriamali, eneo la Iborogero, wilayani Igunga mkoani Tabora, Mei 9, 2014, ikiwa ni sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika muktadha wa ajira kwa vijana.


 Kinana akitazama zao la alizeti alipokagua shamba hilo la alizeti la Vijana la Iborogelo.

HADI KULEEEE KOTE NI SHAMBA LETU: Kinana akimwambia Kinana wakati akimuonyesha shamba hilo la alizeti ambalo limesaidia vijana wa kada mbalimbali kujiajiri.

Katibu Mkuu CCM, Ndugu,Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Bw.Nape (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na vijana wanaoshiriki mradi huo wa kilimo cha alizeti, Iborogero wilayani Igunga mkoani Tabora.

Mwenyekiti wa Vijana SACCOS ya Igunga,mkoani Tabora Bw. Frey Cosseny (wapili kushoto) akiwatambulisha kwa Kinana maofisa wengine wa SACCOS hiyo, Mei 9, 2014 alipofika kukagua shuguli za SACCOS hiyo na kuzungumza na wanachama.

 Katibu Mkuu-CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia Wanachana na Wadau wa SACCOS hiyo.

Kinana akiendesha trekta la mradi wa Igunga Vijana SACCOS,pamoja na mambo mengine alilizindua.

 Kinana akishuka kwenye trekta baada ya kulizindua la Vijana SACCOS ya Igunga,mkoani Tabora.

Katibu Mkuu Kinana akikabidhi funguo kwa mmoja wa Wana-SACCOS hiyo, Joseph Kashindye, wakati alipokagua shughuli za SACCOS hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa wa Tabora, Mei 9, 2014. (Picha zote na Bashir Nkoromo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad