ZIARA UKAWA:-Soma Mabango yaliyotawala katika Mikutano ya UKAWA wilayani Karagwe na Ngara - May 23-24,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 27, 2014

ZIARA UKAWA:-Soma Mabango yaliyotawala katika Mikutano ya UKAWA wilayani Karagwe na Ngara - May 23-24,2014.

Hili ni Bango lililokutwa kwenye mkutano wa UKAWA wilayani Karagwe mkoani Kagera May 23,2014…….Wakati Ukawa wakiendelea na ratiba zao za kuzunguka mikoani, Bunge Maalumu la Katiba limesimama kwa muda hadi mwezi Agosti,2014 kupisha Bunge la Bajeti ambalo linaendelea mjini Dodoma.






…..Bango hili lilikutwa wilayani Ngara mkoani Kagera katika mkutano wa UKAWA-May 24,2014 katika Viwanja vya Posta ya zamani mjini humo…


UKAWA walipotinga wilaya ya Ngara May 24,2014 wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa.


Jukwaa-uwanja wa posta ya zamani mjini Ngara. maandalizi ya Hotuba kutoka kwa UKAWA.


Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiwa wanaendelea kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kudai Katiba ya wananchi, bado viongozi hao wanasisitiza kwamba kamwe hawatarudi kwenye Bunge la Malaamu la Katiba kama njia za kistaarabu za kuwaomba warudi hazitatumika.

Kabla ya kuanza kuzunguka mikoani, Ukawa walianza kampeni za kudai Katiba inayotokana na maoni ya wananchi kupitia Bunge Maalumu la Katiba.

Ukawa wanapinga mchakato huo kutekwa na CCM, kwa madai kuwa wamekuwa wakitumia wingi wao ndani ya Bunge hilo kuchakachua maoni yaliyotolewa na wananchi kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Ziara za viongozi hao wa Ukawa mikoani, zina lengo la kuunganisha nguvu za kudai Katiba ya Wananchi na kuwashirikisha wananchi kuhusu kinachofanywa bungeni.

Vyama vinavyounda Ukawa ambavyo viongozi wake wakuu wanazunguka mikoani ni Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Mosena Nyambambe.

Baadhi ya madai ya Ukawa yanayozungumzwa katika ziara hizo ni mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba na kutekwa kwa wanasiasa kutoka chama kilicho na wajumbe wengi ndani ya Bunge Maalumu la Katiba.

Wakati Ukawa wakiendelea na ratiba zao za kuzunguka mikoani, Bunge Maalumu la Katiba limesimama kwa muda hadi mwezi Agosti kupisha Bunge la Bajeti ambalo linaendelea mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad