PICHA:-Tazama yaliyojiri katika Mahafari ya wahitimu wa Chuo cha Mafunzo ya Madini wilayani Ngara- May 23,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 27, 2014

PICHA:-Tazama yaliyojiri katika Mahafari ya wahitimu wa Chuo cha Mafunzo ya Madini wilayani Ngara- May 23,2014.

Jumla ya wahitimu waliohitimu 14 wamehitimu Masomo yao , wawili kati yao ni wasichana……Chuo kipo maeneo ya Nakatunga karibu na hoteli ya Paradise mjini Ngara na kimesajiriliwa na VETA toka mwaka jana hivyo May 23,2014,Wanafunzi wamehitimu mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kupata ajira sehemu mbalimbali za migodi ya madini hapa nchini.

Mahafari hayo yalianzaa majira ya saa sita mchana tarehe May 23, 2014 chuoni hapo,  ambapo Mgeni rasmi wa sherehe hiyo alikuwa Afisa Elimu kitengo cha Sekondari wa Wilaya ya Ngara pia ikihudhuriwa na wageni wengine ambao ni Mwakilishi wa VATA kanda ya Ziwa , Mlezi wa Chuo cha Nursing Murugwanza , Mkurugenzi wa Chuo hicho ,Bi. Sabrah  pamoja na wageni waalikwa wakiwemo wazazi na wadau mbalimbali.

Akiongea kwenye sherehe hiyo,Mgeni rasmi ameahidi kutoa ushirikiano kwa Wahitimu watakaohitaji mafunzo kwa vitendo migodini kuwasaidia kupata nafasi sambamba na kutoa wito kwa Wazazi na Walezi wilayani Ngara mkoani Kagera na wilaya Jirani kuwapeleke Vijana wao kusoma kwenye vyuo vya ufundi ,maana elimu ni ufunguo wa maisha na vitawasaidia hasa kuwapa Maarifa ya kujitegemea kwa kujiajiri .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad