UMISETA 2014 MKOA WA KAGERA:-Tazama Picha za Matukio yaliyojiri wakati Halmashauri 8 za wilaya za mkoa wa Kagera zilivyoshindana katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Katoke-May 23-27,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 27, 2014

UMISETA 2014 MKOA WA KAGERA:-Tazama Picha za Matukio yaliyojiri wakati Halmashauri 8 za wilaya za mkoa wa Kagera zilivyoshindana katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Katoke-May 23-27,2014.

Timu ya UMISETA kutoka Halmashauri ya wilaya ya Muleba ,mkoani Kagera ikipita kutoa salamu kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera ,Kanal Fabian Massawe wakati wa Mashindano ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa Kagera yaliyo anza May 23 na kumalizika May 27, 2014-kwa kuchezwa michezo ya fainali ili kupata Mabingwa wa Mkoa.





Hawa ni washiriki 71 wa Mashindano ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa Kagera kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ngara ...wakitoa salamu zao kwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi May 24,2014 kwenye Viwanja vya Chuo cha Ualimu Katoke -wilayani Muleba mkoani Kagera.


Picha Juu na Chini......Hawa ni Halmashauri ya wilaya ya Bukoba .......Mashindano ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa Kagera...



Picha katikati ni Mkuu wa mkoa wa Kagera,Fabian Massawe wakifurahia nyimbo kwa pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Mashindano ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa Kagera na Afisa Elimu wilaya ya Ngara Julius Nestor wa pili kushoto,Viongozi wengine na mwisho kulia mwenye shati jeupe ni Afisa Michezo mkoa wa Kagera Kepha Elias wakati wa mashindano hayo yaliyoanza May 23 na kumalizika May 27, 2014-kwenye Viwanja vya michezo vya Chuo cha ualimu Katoke.

...Baadhi ya Viongozi na Wakuu wa Shule za sekondali mbalimbali nao walikuwepo.....kushuhudia Vijana wao wakishindana.....







Kaimu Mwenyekiti wa Mashindano ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa Kagera na Afisa Elimu wilaya ya Ngara Julius Nestor akihutubia wakati wa ufunguzi ambapo alisema UMISETA mwaka huu umeshirikisha Halmashauri zote 8 za mkoa wa Kagera na zimeshindana katika michezo ya Soka,Wavu,Kikapu,Pete,Riadha na Handball.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanal mstaafu Fabiani Masawe akihutubia wakati wa kufungua Mashindano ya michezo kwa umoja wa shule za sekondari Ngazi ya mkoa kwa Mkoa wa Kagera-UMISETA 2014 na kusema kuwa licha ya azma ya Serikali kutekeleza sera ya michezo nchi,wakati umefika sasa kwa Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya mkoani humo nao kuhudhuria Mashindano hayo ya UMISETA  ili kuwa chachu ya kuendeleza michezo katika wilaya zao.


Washiriki wa UMISETA mkoa wa Kagera ambapo wanamichezo 577 kutoka wanafunzi waliochaguliwa katika shule za sekondari za wilaya 8 za mkoa wa Kagera na yana lengo la kupata timu ya UMISETA mkoa wa Kagera wameshiriki-Wilaya hizo ni Manispaa,Bukoba Vijijini,Karagwe,Kyerwa,Misenyi,Ngara,Biharamulo na Muleba.
Mchezo wa RIADHA –ambao unabeba michezo ya Mbio,Mitupo na Miruko ambapo wilaya ya Ngara imefanikiwa kufanya vyema kwa mwaka huu tena kwa kuacha washiriki 7 ambapo Remigius John (mwenye fulana nyeupe) akiibuka mshindi wa kwanza kimkoa katika mbioa za mita 1500 na mita 3000 kwa kuwa mshinidi wa pili.





Katika Mchezo wa WAVU ama Volleyball-Wavulana ,Halmashauri ya Wilaya ya Ngara iliibuka Bingwa wa mkoa UMISETA 2014 kwa kuwafunga Manispaa Bukoba seti 2-0 katika mchezo wa fainali huku ushindi wa tatu ukienda kwa Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo.





Afisa Elimu wilaya ya Ngara Julius Nestor (mwenye suti ya kijivu) akiwa pembeni yake kulia na Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kabanga ...wakifatilia michezo mbalimbali ya UMISETA  2014 Ngazi ya Mkoa wa Kagera.

Katika michezo ya fainali ,Soka Wanaume,Mabingwa wa Mkoa waliibuka Manispaa ya Bukoba kwa kuwafunga Misenyi penati 5-4 na Halmashauri ya wilaya ya Ngara ilifanikiwa kuibuka mshindi wa Tatu wa UMISETA 2014 Ngazi ya Mkoa wa Kagera kwa kuwafunga wapinzani wao wa jadi Biharamulo bao 2-1 katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu.

......Mzee Malimbu nae hakukosekana katika kuisapoti wilaya yake ya Ngara....

Licha ya kiwanja kuwa kibovu ,Katika mchezo wa Kikapu Halmashauri ya wilaya ya Bukoba waliibuka wababe kimkoa  kwa kuwa washindi wa Kwanza,wapili Manispaa na watatu Ngara.


Kwenye mchezo wa NETBALL ,Halmashauri ya wilaya ya Muleba iliibuka Bingwa kwa kuwafunga magoli  19 - 11 Biharamulo na Manispaa Bukoba kuibuka washindi wa tatu.


Mkuu wa mkoa wa Kagera,Fabian Massawe akiwa ni mwana michezo hodari nae hakukosa nafasi ya kuitazama michezo ya Kikapu ,Soka na Wavu iliyokuwa ikichezwa katika viwanja hivyo vya Michezo Katoke.


Mashindano ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa Kagera yamefikia tamati kwa kuchezwa michezo ya fainali ili kupata Mabingwa wa Mkoa.

Katika michezo ya fainali ,Soka Wanaume,Mabingwa wa Mkoa waliibuka Manispaa ya Bukoba kwa kuwafunga Misenyi penati 5-4.

Halmashauri ya wilaya ya Ngara ilifanikiwa kuibuka mshindi wa Tatu wa UMISETA 2014 Ngazi ya Mkoa wa Kagera kwa kuwafunga wapinzani wao wa jadi Biharamulo bao 2-1 katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu.

Aidha Mshindi wa kwanza katika soka la Wanawake ni Manispaa Bukoba akiwanikiwa kumfunga Muleba goli 2-1 huku wa tatu akiwa ni Halmashauri ya Bukoba baada ya kumfunga Misenyi bao 1-0.

Katika Mchezo wa WAVU ama Volleyball-Wavulana ,Halmashauri ya Wilaya ya Ngara iliibuka Bingwa wa mkoa UMISETA 2014 kwa kuwafunga Manispaa Bukoba seti 2-0 katika mchezo wa fainali huku ushindi wa tatu ukienda kwa Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo.

Nao Misenyi waliibuka Mabingwa katika mchezo huo wa WAVU kwa upande wa wasichana wakiifunga Manispaa Bukoba seti 2-0 katika fainali huku Muleba wakishika nafasi ya tatu.

kwa Mujibu wa timu Meneja na Afisa michezo wilaya ya Ngara , Said Salumu amesema kuwa wilaya ya Ngara pia walifanya vyema katika mchezo wa Handball kwa kuibuka Mabingwa wa mkoa UMISETA kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwatandika Biharamulo magoli 15-11 katika mchezo wa fainali huku Manispaa Bukoba wakiambulia nafasi ya tatu-wakati upande wa wanawake wakiibuka Biharamulo wakifuatiwa na Manispaa Bukoba na Muleba.

Kwenye mchezo wa NETBALL ,Halmashauri ya wilaya ya Muleba iliibuka Bingwa kwa kuwafunga magoli  19 - 11 Biharamulo na Manispaa Bukoba kuibuka washindi wa tatu.

Mchezo wa RIADHA –ambao unabeba michezo ya Mbio,Mitupo na Miruko ambapo wilaya ya Ngara imefanikiwa kufanya vyema kwa mwaka huu tena kwa kuacha washiriki 7 ambapo Remigius John akiibuka mshindi wa kwanza kimkoa katika mbioa za mita 1500 na 3000 mshinidi wa pili huku Neema Venansi akiibuka mshindi wa pili kimkoa kwa wasichana katika mbio za mita 1500  na Vitalis Petter akifanya vyema kwa mita 800.

Katika mchezo wa Kikapu wilaya ya Ngara iliibuka mshindi wa tatu kwa kuifunga Misenyi vikapu 30-12 ambapo Halmashauri ya wilaya ya Bukoba waliibuka wababe kimkoa  kwa kuwa washindi wa Kwanza,wapili Manispaa na watatu.

Said Salumu amesema  wilaya ya Ngara kwa mwaka huu imefanikiwa kutoa washiriki 18 kuunda kikosi cha UMISETA ngazi ya mkoa ,kitakachopambana na Mkoa wa Geita kuanzia May 31,Mwaka huu katika Mashindano ya Kanda kati ya mkoa wa Kagera na Mkoa wa Geita ili kupata timu ya Kanda ya ziwa Magharibi itakayoshiriki mashindano ya UMISETA ngazi ya Taifa ya siku 11 -kuanzia June 9 ,mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad