Waziri wa
Fedha wa Tanzania,Mhe. Saada Mkuya Salum akiwasilisha Mapendekezo ya Mfumo wa
Mapato na Matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15 kwa Waheshimiwa
Wabunge.
|
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais - Uhusiano Mhe. Steven Wazira akiwasilisha mwelekeo wa hali
ya uchumi kwa mwaka 2014/2015 kwa waheshimiwa wabunge.
|
Wabunge
wakifuatilia hotuba kwa makini.
|
Watendaji wa
Wizara ya Fedha wakimsikiliza Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum…Picha na
Owen Mwandumbya.
|
Serikali
imetoa mwelekeo wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2014/15 kuwa ni Sh19.6 trilioni,
ikilinganishwa na Sh18.2 za Bajeti iliyopita.
Vipaumbele
vya Bajeti hiyo ni kuendeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulioanza
mwaka 2011 na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao unajumuisha maeneo
sita ya kitaifa ya kilimo, elimu, maji, utafutaji wa rasilimali fedha, nishati,
uchukuzi na uboreshaji wa mazingira ya kufanyia biashara.
Katika
kuhakikisha inakusanya fedha za kutosha, Serikali imeahidi kuunda kikosi kazi
cha kufuatilia mapato yote yanayotoka halmashauri zote nchini ili kuondoa
visingizio vilivyojitokeza wakati wa ufuatiliaji wa mapato.
Hayo
yalielezwa jana(April 30,2014) na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya wakati akiwasilisha mapendekezo
ya Bajeti hiyo kwa kamati zote za Bunge, Dar es Salaam.
Alisema
matumizi ya kawaida kwa mwaka ujao wa fedha yanalenga kufanikisha mambo 20
muhimu, yakiwamo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014, Uchaguzi Mkuu 2015,
kukamilisha mchakato wa Katiba na nyongeza ya mishahara na kulipa kwa wakati.
Mkuya
alisema makadirio ya matumizi ya maendeleo ni Sh7.7 trilioni sawa na asilimia
39 ya matumizi yote ya Serikali.
Kati ya
fedha hizo, miradi ya maendeleo imetengewa Sh5.4 trilioni sawa na asilimia 27
na matumizi mengine ya maendeleo ni Sh2.2 trilioni.
Utegemezi.
Mkuya
alisema katika mwaka unaomalizika, Serikali ilipanga kukopa Dola 700 milioni za
Marekani sawa na Sh1.1 trilioni na kati ya kiwango hicho, iliambulia mkopo wa
Dola 259 milioni hivyo kuweka nakisi ya Dola 441.
Alisema
katika mwaka wa fedha 2014/2015, Serikali imekusudia kukopa Sh4.2 trilioni
kutoka vyanzo vya mapato vya ndani na nje ili kuziba pengo la mapato.
Misaada na
pato la taifa.
Katika mwaka
wa 2013/2014, Serikali ilipokea misaada ya Sh1.1 trilioni kutoka kwa washirika
wa maendeleo ikiwa ni asilimia 50 ya ahadi ya Sh2.3 trilioni, hivyo kuweka
nakisi ya Bajeti ya Sh1.2 trilioni.
Akiwasilisha
Rasimu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2014/2015, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema deni la Taifa limefikia
Sh27.04 trilioni kutoka Sh24 trilioni na kufafanua kuwa ongezeko la deni hilo
limetokana na mikopo mipya ya kibiashara na ya masharti nafuu.
Ukusanyaji
mbovu wa mapato.
Akizungumzia
ukusanyaji wa kodi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kumekuwa na matatizo
katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, hasa yasiyotokana na kodi.
No comments:
Post a Comment