Fernando
Torres alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya 36 kwa pasi ya Azpilicueta baada
ya kazi nzuri ya Willian, lakini Adrian Lopez akaisawazishia Atletico dakika ya
44 kwa pasi ya Juanfran.
|
Kwa kufungwa
bao 3-1 sasa Chelsea imeaga Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2013/2014 na Atletico
sasa itakutana na jirani zao, Real Madrid katika fainali May 24,2014, nchini
Ureno, ambao nao April 29,2014, waliwang’oa mabingwa watetezi, Bayern Munich
kwa 4-0 mjini Munich na kufanya ushindi wa jumla wa 5-0.
Fainali hiyo
itazikutanisha timu za mji wa Madrid, zote zikiwa na jina la Madrid na zina
upinzani mkubwa kisoka, hivyo Real Madrid wanaingia katika fainali hiyo na Kombe
lao la 9 la Ulaya, na sasa wanasaka Taji la 10 ambalo wenyewe wamelibatiza ‘LA
DECIMA’.
Diego Costa akafunga bao la pili kwa penalti dakika ya 61 kabla ya Arda Turan kumaliza kazi dakika ya 72 na Atletico imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza Madrid wiki iliyopita.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Jose Mourinho dakika ya 54 kumtoa beki Ashley Cole na kumuingiza mshambuliaji Samuel Eto’o ndiyo yaliigharimu Chelsea. Eto’o ndiye aliyesababisha penalti iliyofungwa na Costa.
No comments:
Post a Comment