Akiingizwa
kwenye gari la wagonjwa tayari kwa kupelekwa hospitali kwa hatua zaidi.
|
Baadhi ya
jamaa na Wafanyakazi wenzake aliyoambatana nao wakimwangalia mara baada ya kufikishwa chumba cha
huduma ya kwanza.
|
Mmoja wa
watu aliokuwa nao ambaye yaelekea ni mfanyakazi mwenzake akiwa anaingia katika
gari hilo huku akiwa amebeba nguo na viatu vya Rashid John Chilwangwa.
|
Gari la
wagonjwa lililombeba likiondoka uwanjani leo May 1, 2014 kuelekea hospitali.
|
Maadhimisho
ya Siku ya Wafanyakazi Kitaifa, maarufu kama Mei Mosi yaliyofanyika leo –May 01,2014,Jijini
Dar es Salaam yameingia dosari baada ya mmoja wa wafanyakazi kufariki dunia
uwanjani kwa ghafla akiwa katika maadhimisho hayo.
Mfanyakazi
huyo anayedaiwa kufanya kazi Ikulu, alizidiwa ghafla akiwa katika maandamano na
kupatiwa huduma za kwanza lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na hatimaye
kudaiwa kupoteza maisha akipatiwa huduma na madaktari na wahudumu kutoka kikosi
cha msalaba mwekundu waliyokuwa katika maadhimisho hayo.
Thehabari.com
ilishuhudia mfanyakazi huyo akiletwa katika kambi ya watu wa huduma ya kwanza
iliyokuwa katikati ya uwanja wa Uhuru, kisha kupatiwa huduma ya kwanza bila
mafanikio na baadaye alifariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kundi
ambalo lilimleta mfanyakazi huyo baada ya kuzidiwa ghafla lilimtaja kuwa jina
lake ni Rashid John Chilwangwa.
Mmoja wa
wafanyakazi waliyokuwa wameandamana na mfanyakazi huyo ambaye hakupenda kutaja
jina lake kwa kuwa yeye si msemaji akisimulia tukio hilo, alisema John
Chilwangwa (45) walikuwa naye katika sherehe za maadhimisho na hali yake
ilibadilika kabla ya kuingia uwanjani na aliomba aende kujisaidia haja ndogo
baada ya hapo alianza kuishiwa nguvu.
“…Si
tulishangaa alikaa muda kidogo akijisaidia baada ya kumfuata tulimkuta ametoka
ndani ya choo na kuja nje na kisha kukaa kwenye tofali huku akisema anajisikia
kuishiwa nguvu na hali ilibadilika ndo tukamleta hapa,” alisema shuhuda huyo.
Alipoulizwa
hali yake kwa sasa ambapo alikuwa ameingizwa kwenye hema la huduma ya kwanza
kwa wahudumu kutoka kikosi cha msalaba na madaktari alisema wamejaribu
kumuhudumia lakini bahati mbaya amefariki dunia tayari.
“…Tumeambiwa na
madaktari kuwa ameshafariki tayari,” alisema shuhuda huyo ambaye alikuja na
mgonjwa huyo.
Mwandishi wa
habari hizi alishuhudia madaktari wakijaribu kumtundikia dripu huku wakijaribu
kurudisha mapigo ya moyo kwa kushtua mara kadhaa lakini juhudi ambazo hazikuzaa
matunda.
Baada ya kubaini amefariki dunia walisita kumwekea dripu ambayo
ilikuwa inaandaliwa na badaye walimfunika kwa shuka nyeupe na kuita gari la
wagonjwa tayari kwa kumpeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi. Hata hivyo
hakupatikana mara moja daktari kuzungumzia kilichomsibu Chilwangwa.
Habari Na:- Thehabari.com
No comments:
Post a Comment