VPL 2013 / 2014:-Baadhi ya washindi wa ligi kuu Tanzania bara 2013/2014 -Timu bora, Kipa bora, Mfungaji bora na Pesa walizozawadiwa..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 28, 2014

VPL 2013 / 2014:-Baadhi ya washindi wa ligi kuu Tanzania bara 2013/2014 -Timu bora, Kipa bora, Mfungaji bora na Pesa walizozawadiwa..’’


Baadhi ya zawadi ni kama zinavyoonekana katika utoaji wa Zawadi na tuzo zimetolewa kwa timu zilizofanya vizuri na wachezaji waliong’ara msimu wa ligi kuu ya Vodacom 2013/2014 na kukabidhiwa zawadi kwa thamani ya pesa na vikombe Jana May 27,2014 na mdhamini wa ligi hiyo ambae ni Vodacom Tanzania.

Kwenye usiku huo Vodacom Tanzania imetoa jumla ya milioni mia mbili sitini na mbili (262,000,000) kwa washindi wote ligi kuu.

Mwakilishi wa mchezaji bora msimu wa mwaka 2013/2014 ambaye ni Kipre Tchetche wa @azamfc akichukua zawadi kwa niaba. #VPL2014 Winner


Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania akizungumza katika hafla hii. #VPL2014Winners.


Rais wa TFF Jamal Malinzi anazungumza sasa kuhusiana na mwenendo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.

Anasema Ndanda kumekucha na Stand Pia wapo juu.

Changamoto wanazokumbana nazo TFF ni viwanja vibofu,waamuzi wabovu,fujo,uhuni na vitendo vya kishirikina viwanjani-Bodi ya Ligi.

Jumla ya hat tricks zilizofungwa msimu huu ni 4 ambapo msimu uliopita hakukuwa na hat trick hata moja.

Bingwa wa mwaka huu ana pointi 2 zaidi ya bingwa wa mwaka jana na magoli yamefungwa mengi zaidi kwa wastani wa 2.2 kwa mechi.

Timu zinazopata zawadi leo ni @azamfc @Yanga1935 @MbeyaCityFC na @SimbaSC36 #VPL2014 #VPL2014Winners


Wadau wa mpira wakifuatilia hotuba ya Rais wa TFF Jamal Malinzi #VPL2014Winners #VPL2014
Azam FC Bingwa wa #VPL2014 wanapata kitita cha Tsh 75 Mil  na Yanga SC 1935 wanapata Tsh 35 Mil kwa kuibuka washindi wa pili msimu wa mwaka 2013/2014.

Kocha bora msimu wa 2013/2014 ni Juma Mwambusi wa Mbeya City FC, golkipa bora msimu wa mwaka 2013/2014 ni Hussein Sharifu wa Mtibwa Sugar anapata zawadi ya Tsh 5,200,000 na tuzo.

Mchezaji bora msimu wa mwaka 2013/2014 ni Kipre Tchetche wa @azamfc anapata Tsh 5.2M, mfungaji bora msimu wa mwaka 2013/2014 ni Amisi Tambwe wa @SimbaSC 36 

Mwamuzi bora msimu wa 2013/2014 ni Israel Mjuni ambapo timu yenye nidhamu msimu wa mwaka 2013/2014 ni Yanga SC ambayo imezawadiwa Tsh 16M.

Majina ya washindi na zawadi zao ni kwa mujibu wa @VodacomTanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad