![]() |
Msanii , Rachel Haule 'Recho'enzi ya uhai wake
aliyefariki jana (May 27,2014)saa mbili
usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
|
![]() |
Mume wa Rachel aitwaye Saguda akiwa na majonzi.
|
![]() |
Huzuni tele ikiwa imetawala wasanii waliokuwa viwanja ya Leaders.
|
![]() |
Steve akizungumza na wanachama wa
Bongo Muvi, viwanja vya Leaders.
|
MASTAA wa Bongo Muvi wamemlilia msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho' aliyefariki jana (May 27,2014)saa mbili usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kujifungua ambapo mtoto wake alifariki muda mfupi na baadaye yeye akafariki.
Kwa mujibu wa
mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve ‘Nyerere’, mwili wa Rachel utasafirishwa kwenda
kwao Songea kwa ajili ya maziko.
Taarifa zinasema Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
Shughuli ya
kuagwa kwa mwili itafanyika kwenye viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni na
pia siku hiyo yatafanyika mazishi ya wote wawili yaani mama pamoja mtoto.
Taarifa ya
mwanzo ya familia ilikua marehemu akazikwe kwao Songea lakini kutokana na
ushawishi wa waigizaji imebidi familia ya Rachel ikubaliane na ombi lao la
maziko kufanyika Dar es salaam.
Recho
alianza rasmi kuingia katika sanaa ya maigizo mwaka 2009, katika kikundi cha
Mburahati, kabla hajajiingiza rasmi kwenye uigizaji wa filamu.
Moja ya sifa
zilizomfanya kujulikana, ni tabia ya kupendelea kuvaa nguo fupi, jambo ambalo
alipohojiwa, alisema zinamfanya ajisikie huru na amani pindi anapofanya
shughuli zake.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movie ,Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mshtuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo.
Mwanawamakonda Blog ...'' Inatoa pole kwa familia na wasanii wote ..''
poleni sana kwa msiba watanzania wote na hasa wanafamilia misiba miwili kwa pamoja...Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipendi hiki cha huzuni.
ReplyDelete