Polisi wakiwa wamefika eneo la klabu ya simba
ili kuimarisha ulinzi na kuwataka wanachama wa simba kutulia ili wapate majibu
kwa kamati ya uchaguzi.
|
Wanachama wa simba wakiwa wamelizunguka Jengo
la klabu yao mchana huu kupinga kuondolewa kwa wambura kwenye uchaguzi wa klabu
hiyo.Picha na Sek David
|
Michael Richard
Wambura aliyekuwa anawania nafasi ya uenyekiti katika klabu ya Simba kupitia
uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Juni 29, jijini Dar es Salaam, amechujwa
katika mbio hizo kwa kutokuwa mwanachama.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi, Damas Ndumbaro, amesema Wambura ameenguliwa kwa
kutokidhi matakwa ya kanuni zinazotumika katika mchakato huo kutokana na dosari
katika uanachama wake.
Ndumbaro
alisema kutokana na Wambura kuvuliwa uanachama wake mwaka 2010 kwa kosa la
kuishitaki Simba mahakamani, jambo hilo lilipaswa kupelekwa kwenye mkutano mkuu
wa wanachama kwa uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa ibara ya 55 ya katiba ya klabu
hiyo.
Alisema
kamati yake ilipokea barua tatu kutoka kwa Wambura, ikiwemo ya Desemba 12,
mwaka 2012 kwenda kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage akiomba kuelezwa hatma
ya uhalali wa uanachama wake na akajibiwa kuwa ingefanyiwa kazi.
Ndumbaro
ambaye ni mwanasheria kitaaluma, alisema kwa mazingira hayo, kamati yake
ilibaini kuwepo kwa mchanganyiko wa barua hizo na kudai kusema Ibara ya 12 ya
Simba, mwanachama aliyesimamishwa uanachama anakosa haki ya msingi ya kushiriki
uchaguzi, iwe kuchaguliwa au kuchagua.
Kati ya
wagombea waliokuwa wakipingwa, Wambura alikuwa akiongoza kwa kupingwa na
wanachama watano; Said Lubea, Ustadh Masoud, Jackson Chacha, Varentino Nyaru na
Swalehe Madjaba, lakini baadhi ya pingamizi zilitupwa kwa kukosa nguvu ya hoja.
Mbali ya
Wambura, wagombea wengine waliokuwa wamepingwa ni Geofrey Nyange ‘Kaburu’,
Swedy Nkwabi na Joseph Itang’are ‘Kinesi’ kwa nafasi ya makamu pamoja na Aveva
anayewania nafasi ya rais.
Wengine
waliokuwa wakipingwa ni Ibrahim Masoud ‘Maestro’, Said Pamba, Chano Almas na
Daniel Manembe wanaowania nafasi ya ujumbe, ambao wote wamepenya kutokana na
kufanikiwa kupangua pingamizi dhidi yao.
Akizungumzia
kuenguliwa kwake, Wambura alisema ni kitu ambacho alikitarajia kutokana na
dalili kujitokeza mapema katika mchakato huo kwa lengo la kumkwamisha, lakini
atapambana kwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwani ni mwanachama halali wa
klabu hiyo.
Uchaguzi huo
umepangwa kufanyika Juni 29, kuhitimisha zama za Alhaji Ismail Aden Rage
aliyeingia madarakani Mei 9, 2010.
No comments:
Post a Comment