 |
Mtuhumiwa alipofikishwa Mahakamani hapo (May 27,
2014) ambapo MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea mashtaka raia wa Nigeria,
Olabisi Ibidun Cole (65) ya tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya gramu
831.94 zenye thamani ya shilingi za Kitanzania milioni 37.4.
|
 |
Mwendesha Mashtaka, Jackson Chidunda, alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa
mahakama hiyo, Frank Mushi, kuwa mshtakiwa anakabiliwa na tuhuma za
kusafirisha dawa za kulevya alipokamatwa Mei 19, 2014, Cole akiwa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alipokutwa na madawa aina ya
heroin.
|
Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa
upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo itasomwa tena katika mahakama hiyo Juni 10 mwaka huu na
mshtakiwa amerudishwa rumande.
Chanzo:- GPL
No comments:
Post a Comment