![]() |
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova Kova alisema hakuwa
amepokea taarifa yoyote ya aina hiyo..PICHA|MAKTABA.
|
Mume wa
mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, (jina tunalihifadhi kwa sasa),
anatuhumiwa kumbaka shemeji yake mdogo (17).
Taarifa za
tukio hilo ziliripotiwa juzi saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata
(Tabata Shule), zikimtuhumu mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu
na kumsababishia maumivu makali.
Binti huyo
alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili ambao
walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa mtuhumiwa wa
kuzima kesi hiyo.
Akizungumza
na gazeti hili nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye alimbaka mara
ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alipombaka mara mbili ndani ya gari.
Alisema mara
ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba angemdhuru kama
angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa sebuleni nyumbani kwako
Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa ndugu zake baada ya kubakwa
mara ya pili.
Polisi
katika kituo hicho walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo lakini
walishindwa kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa maelezo kwamba hawakuwa na askari wa
kutosha na kuahidi kwamba angekamatwa jana. Hata hivyo, hadi jana mtuhumiwa
huyo alikuwa hajakamatwa.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kutwa nzima ya jana hakupatikana
kuzungumzia tukio hilo na kila simu yake ilipopigwa (kati ya saa nane mchana na
saa mbili usiku), ilipokewa na msaidizi wake akisema bosi wake ana kazi
nyingine.
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hakuwa amepokea
taarifa yoyote ya aina hiyo.
Mwimbaji
anena.
Alipoulizwa
jana, mwimbaji huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kwa undani tuhuma
zinazomkabili mumewe na kwamba alikuwa anajisikia vibaya kutokana na tukio hilo
kuhusisha watu wake wa karibu.
“Of course
(bila shaka), hili sio tukio zuri. Kwa sasa sina uwezo wa kuzungumza kwa sababu
hili suala lipo Polisi.
I am confused (nimechanganyikiwa), ukizingatia kwamba
linasemekana kutokea wakati sikuwepo nyumbani, naomba tuzungumze baada ya akili
kutulia,” alisema.
Kadhalika,
jana saa 6:20 mchana, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mtuhumiwa ambaye
baada ya kupewa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili alisema: “Samahani sana
ujue sikusikii kabisa,” kisha alikata simu.
Habari Na:-Mwananchi.
No comments:
Post a Comment