![]() |
Hatimaye mikutano ya UKAWA imeanza rasmi mkoa wa Kigoma, leo(May
28, 2014) mkutano umefanyika Kasulu mjini.
|
Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umesema kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
Kanal Mstaafu Issa Machibya kuzuia kwa
Muda mikutano ya Umoja huo kimewasababishia Hasara ya Kisiasa
Mratibu wa ziara ya UKAWA kwa Mikoa ya Kanda ya Magharibi,Bw. Peterson
Mushenyera akizungumza na Radio Kwizera FM,amesema kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa walilazimika kutofanya
mikutano kwa takribani siku nne jambo ambalo ni kinyume na malengo ya ziara yao
ambapo kwa kipindi walichozuiwa walikuwa wakifanya mikutano ya ndani kwa
kuzungumza na Viongozi wote wa Vyama vinavyounda UKAWA,watu mashuhuri,Viongozi
wa dini pamoja na watu mbalimbali wakielimishwa kuhusu rasimu ya pili ya
Katiba,hoja na nia ya kuwa na Serikali 3.
Amesema baada ya kupewa ruhusa ya kuendelea na Mikutano hiyo sasa
wataanzia Kasulu mjini hii leo (May 28, 2014),May 29,kabla ya kuhitimisha May
31,2014 mjini Kibondo.
Kesho May 29, 2014-UKAWA utakuwa wilayani Buhigwe katika eneo la Muyama
na May 30,2014 watakua na mkutano Kigoma Mjini.
Hivi karibuni Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya Hadhara ya Umoja wa
Katiba ya wananchi (UKAWA) kufanya mikutano yao mkoani Kigoma na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma alisema
mikutano hiyo imepigwa marufuku kwa usalama wa viongozi wa Ukawa.
Itakumbukwa kwamba katibu mkuu wa
NCCR-Mageuzi,Bw.Mosena Nyambabe alitiwa mbaroni na Jeshi la Polisi katika kijiji
cha Nguruka wilaya ya Uvinza ,mkoani humo kwa tuhuma ya kuwadhalilisha viongozi
wa Kitaifa na kuachiwa huru kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment