Katibu mkuu wa CHADEMA ,Dr. WILBROAD SLAA akizungumza na wanahabari mapema jana (May 12,2014) juu ya ziara yao ya nchi nzima.
|
Umoja wa Katiba ya Watanzania UKAWA jana(May 12,2014) umejitokeza na kutangaza rasmi
ratiba yao ya kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu juu ya katiba mpya
na mchakato huo ulipofikia sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya makao makuu ya Chama cha Wananchi CUF ,katibu mkuu
wa CHADEMA ,Dr. WILBROD SLAA amesema kuwa UKAWA sasa imeanza rasmi kufanya
maandamano na mikutano nchi nzima kila kona ya Tanzania kwa lengo la kuwafikia
wananchi na kuwaeleza ukweli kuhusu mchakato wa katiba.
Katibu mkuu wa NCCR mageuzi MOSENA NYAMBABE akizungumza ambaye ni mmoja
kati ya viongozi wa UKAWA ambao watazunguka nchi nzima ,pamoja na mambo mengine kuelezea mchakato wa Katiba Mpya.
|
Dr. SLAA anasema kuwa kwa wale ambao wanasema kuwa UKAWA ni nguvu ya soda
wanapotea, kwani muungano huo haujaja kwa bahati mbaya kwani wamejipanga kuhakikisha
kuwa inawaeleza Watanzania ukweli juu ya katiba na jinsi chama cha mapinduzai
CCM wanavyoupotosha umma juu ya mchakato huo.
Aidha Dr. SLAA amesema
kuwa kauli ambazo zilitolewa na viongozi wa juu wa chama cha
mapinduzi CCM kuwa Tanzania haiitaji sana katiba mpya ni kauli za mtu ambaye
hajafika darasani na ni kuwapotosha watanzania na kauli hizo zinatakiwa kupigwa
vita sana kwani zinaupotosha umma.
JULIUS MTATIRO akizungumza katika mkutano huo.
|
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mkutano huo wa UKAWA
na wanahabari jana May 12,2014.
|
UKAWA wametangaza kufanya maandamano na mikutano kona zote za Tanzania
kwa kuigawa Tanzania kwa kanda tatu ambazo ni KANDA YA KATI,KANDA YA KASKAZINI
na KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI,ambapo viongozi kutoka vyama vitatu wakiwemo
makatibu wakuu wote wataongoza mikutano hiyo ambayo itaanza rasmi tarehe 14 ,May
,2014.
"UKAWA
INAANZA TANZANIA BARA" RATIBA YA ZIARA YA AWAMU YA KWANZA YA UKAWA, TAREHE
14 - 27 MEI
2014.
TIMU “A”-
KANDA YA KAT.
1. Mhe.
Mosena Nyambabe (NCCR) – Katibu Mkuu.
2. Mhe.
Ashura Mustapha (CUF) – Mjumbe wa Baraza Kuu.
3. John
Heche (CHADEMA) – Mwenyekiti wa Vijana Taifa.
TAREHE ENEO
LA MKUTANO.
Tarehe
14/05/2014 MOROGORO MJINI.
Tarehe 16/05/2014 SHINYANGA MJINI.
Tarehe 17/05/2014 BARIADI MJINI.
Tarehe 18/05/2014 NZEGA MJINI.
Tarehe 19/05/2014 TABORA MJINI.
Tarehe 20/05/2014 URAMBO.
Tarehe 22/05/2014 NGURUKA.
Tarehe 23/05/2014 KIGOMA MJINI.
Tarehe 24/05/2014 MNANILA.
Tarehe 25/05/2014 KASULU MJINI.
Tarehe 26/05/2014 KASULU VIJIJINI.
Tarehe 27/05/2014 KIBONDO MJINI.
TIMU “B”
– KANDA YA KASKAZINI.
1. Dr
Willibroad Slaa(CHADEMA) – Katibu Mkuu.
2. Mhe. Mustapha Wandwi (CUF) – Mjumbe
wa Baraza Kuu.
3. Ahmed Msabaha (NCCR) – Mjumbe
wa Halmashauri Kuu.
TAREHE ENEO
LA MKUTANO.
Tarehe 14/05/2014 MOSHI MJINI.
Tarehe 15/05/2014 BABATI MJINI.
Tarehe 16/05/2014 ARUSHA MJINI.
Tarehe 18/05/2014 MUSOMA MJINI.
Tarehe 19/05/2014 TARIME MJINI.
Tarehe 20/05/2014 BUNDA MJINI.
Tarehe 21/05/2014 BIHARAMULO MJINI.
Tarehe 22/05/2014 BUKOBA MJINI.
Tarehe 23/05/2014 KARAGWE MJINI.
Tarehe 24/05/2014 NGARA MJINI.
Tarehe 25/05/2014 KATORO.
Tarehe 26/05/2014 GEITA MJINI.
TIMU “C”
– NYANDA ZA JUU KUSINI.
1. Prof.
Ibrahim Haruna Lipumba(CUF) – Mwenyekiti.
2. Mhe. Said Issa (CHADEMA) – Makamu
Mwenyekiti Taifa.
3. Martin Juju Danda(NCCR) – Mjumbe
wa Halmashauri Kuu.
TAREHE ENEO
LA MKUTANO.
Tarehe 15/05/2014 IRINGA MJINI.
Tarehe 16/05/2014 MAFINGA.
Tarehe 17/05/2014 MAKAMBAKO MJINI.
Tarehe 18/05/2014 NJOMBE MJINI.
Tarehe 19/05/2014 SONGEA MJINI.
Tarehe 20/05/2014 MBINGA MJINI.
Tarehe 22/05/2014 MBEYA MJINI.
Tarehe 23/05/2014 MOMBA.
Tarehe 24/05/2014 SUMBAWANGA MJINI.
Tarehe 25/05/2014 NAMANYERE.
Tarehe 26/05/2014 KATAVI MPANDA - MULELE (MAJIMOTO).
Tarehe 27/05/2014 MPANDA MJINI.
Aidha UKAWA
umewataka wananchi wa maeneo yote yaliyotajwa mjiandae na awamu ya kwanza ya
ziara hii. Awamu ya pili itaendelea mwezi Juni na ziara za wabunge
walioko bungeni mtatangaziwa.
No comments:
Post a Comment