![]() |
Wananchi
wenye mabango wakiwa pamoja katika mkutano wa UKAWA wilayani Ngara mkoani Kagera May 24,2014 ili Dr Slaa aweze kusomwa ujumbe wakati
aliposimama kuhutubia wananchi wa Ngara mkoani Kagera.
|
![]() |
Picha juu na chini ,Kijana
Inocent John akionesha bango la kupinga serikali tatu katika mkutano wa UKAWA
wilayani Ngara mkoani Kagera -Mei 24,2014.
|
Hali hiyo ilijitokeza
kwenye mkutano huo wakati mjumbe wa baraza kuu la CUF Bw.Mustafa Wandwi akihutubia
wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa UKAWA huku akiwahamasisha kujitokeza kupiga kura za maoni
kupendekeza serikali tatu katika rasimu ya katiba mpya.
Inocent John
alionesha bango lisemalo ...''Wananchi wana matatizo mengi na Serikali tatu sio
suluhisho hivyo ziendelee serikali mbili ..'' lakini alipotakiwa kutetea maoni yake
alianza kusua saua na kujibu mambo ambayo sio matatizo ya wananchi.
Hata hivyo
Dr Wilbroard Slaa amewataka vijana kuwa makini na wanasisa wanaopinga maendeleo
na haki za binadamu kwani kijana huyo alipewa bango na wanachama wa CCM ili
kuvuruga mkutano huo bila yeye kuwa na utambuzi.
No comments:
Post a Comment