MAZISHI YA RECHO:- Safari ya mwisho akizikwa katika makaburi ya Kinondoni leo May 29, 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 29, 2014

MAZISHI YA RECHO:- Safari ya mwisho akizikwa katika makaburi ya Kinondoni leo May 29, 2014.

........Majeneza yenye miili ya Recho na mwanaye.......Mwili wa muigizaji wa filamu nchini Rachel Haule umeagwa leo (May 29, 2014) hii katika viwanja vya Leaders na baada ya hapo amezikwa katika makaburi ya Kinondoni. Wasanii wengi ndugu, jamaa na marafiki wamejawa katika simanzi kubwa huku Irene Uwoya akizimia pengine kwa mshituko wa kuondokewa na msanii mwenzao.

Miili ya Rachel Haule 'Recho' na mwanaye ikishushwa kwenye gari maalum baada ya kuwasili Viwanja vya Leaders ikitokea nyumbani Palestina, Dar es Salaam tayari kwa kuagwa.




RECHO: Hapa ndipo atakapo anza siku yake ya kwanza leo (May 29,2014) kwenye makazi yake mapya mbinguni. Shimo dogo ni kaburi ya mtoto wake aliyefariki muda mfupi baada ya kumzaa!

RECHO: KUZALIWA 1988  KUFARIKI: 2014. UMRI: 26 yrs.

KUAMBIANA: Hapa ndipo yalipo makazi ya milele ya Adam Kuambiana aliyefariki wiki iliyopita, leo ( May 29,2014 ) akitimiza siku ya 13 kwenye makazi yake mapya.

KUAMBIANA: KUZALIWA:  1976 - KUFARIKI: 2014  UMRI: 38 yrs.

JOHN MAGANGA: Haya ni makazi ya John Maganga akiwa leo naye anatimiza mwaka mmoja na miezi 6.

JOHN: KUZALIWA: 1988 KUFARIKI: 2012 UMRI: 24 yrs.

MALISA: Haya ni makazi ya milele ya msanii mwingine Malisa ambaye ameshatimiza mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu atutoke.

ZUHURA: KUZALIWA: 1974 KUFARIKI: 2013 UMRI: 39 yrs.

 KANUMBA: Haya ni makazi ya milele ya Kanumba ambaye sasa ana miaka 2 na miezi 2.

KUZALIWA: 1984 KUFARIKI: 2012 UMRI: 28 yrs.



Hakika vijana wengi hivi sasa wanaondoka duniani mapema mno, wakiwa na umri chini ya miaka 30 na 40. 

Mfano hai ni wasanii maarufu wa Bongo Movie waliokwisha tutoka ndani ya kipindi cha miaka miwili wakati leo tunamzika Recho, kama yanavyojionesha makaburi yao, ambao wate wamelazwa sehemu moja ya Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

HAKIKA MBELE YAO, NYUMA YETU. MUNGU AZILAZE ROHO ZAO PEPONI - AMEEN!

(Picha za makaburi ni za leo-May 29,2014, zimetumwa Global WhatsApp na: Shani Ramadhani na Imelda Tarimo/GPL)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad