![]() |
Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasabahi wananchi wa kijiji cha Nyumbigwa wilayani
Kasulu,mkoani Kigoma leo (April 09,2014) walipofika na Ujumbe wake Kukagua
mradi wa maji.
|
![]() |
Mbunge wa
Viti Maalum Josephine Gezabuke akizungumza na wananchi wakati waziara ya Katibu Mkuu Ndugu
Abdulrahman Kinana kukagua mradi wa maji wa kijiji cha Nyumbigwa .
|
![]() |
Tanki la
maji la kijiji cha Nyumbigwa lina uwezo wa kubeba lita 290,975 na kuwahudumia
zaidi ya watu elfu 11.
|
Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi Bw Abdulrahman Kinana amewataka wakazi wa wilaya ya
Kasulu Mkoani Kigoma kuepuka Itikadi zao za kisiasa katika utekelezaji wa
miradi ya maendeleo katika maeneo yao
Bw Kinana
ametoa wito huo leo(April 09,2014)
alipokuwa akikagua ujenzi wa Mradi wa Maji unaoendelea katika Kijiji cha
Nyumbigwa wilayani Kasulu katika siku ya kwanza ya ziara yake wilayani humo.
Amesema kuwa
miradi yote inayojengwa kwenye vijiji vya wilaya hiyo ina lengo la kutatua
changamoto zinazowasibu wakazi wa maeneo husika bila kujali itikadi ya vyama
vyao vya siasa, dini, kabila wala rangi zao.
Aidha Bw
Kinana ametoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo
iliyosomwa na mhandisi wa Maji wilayani humo Bw Mbaraka Rajab aliyesema kuwa
mradi huo haujakamilika kwa wakati kutokana na baadhi ya wanasiasa kuingizwa
masuala ya kisiasa.
Habari
Na:-Radio Kwizera FM.
No comments:
Post a Comment