AJALI:-Taswira ya Gari Toyota RAV 4 ilivyoteketea kwa Moto eneo la Selander Bridge Jijini Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 10, 2014

AJALI:-Taswira ya Gari Toyota RAV 4 ilivyoteketea kwa Moto eneo la Selander Bridge Jijini Dar es Salaam.


Gari hili aina ya Toyota Rav 4 likiteketea kwa moto maeneo Selander Bridge jijini Dar es Salaam jana.(April 09,2014) huku mmiliki wake baada ya ajali hiyo hakuweza kuongea lolote zaidi ya kulia.




Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza mara baada ya kufika  eneo la tukio,walisema kuwa waliona watu wakikimbia ovyo baada ya kutanda kwa moshi mkali na baadae waliona moto ukizuka ila inaonekana chanzo cha ajali hiyo ni hitrafu ya umeme kwenye gari hilo.



Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa na gari hilo liliteketea kwa moto Aprili 9, 2014 katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad