Ndugu Kinana
na Msafara wake ulikuwa umetoka kijiji cha Namanyere kuelekea kijiji cha
Mwampemba kusikiliza matatizo ya Wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo iliyopangwa kutekelezwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.
Barabara
hiyo yenye urefu wa kilometa 100,lakini iliwachukua zaidi ya masaa 12 kwenda na
kurudi kutokana na ubovu wa barabara.
Ndugu Kinana yuko Mkoani Rukwa,Katavi na
Kigoma kwa ziara ya siku 21 ya kuimarisha Chama cha CCM,kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo kiwemo na kuzisikiliza kero mbalimbali za wananchi.
![]() |
|
Hali ilikuwa
tete mnoo,kipande cha kilometa mia kinapitika kwa zaidi ya masaa sita,kutoka
kijiji kimoja kwenda kingine.
|
![]() |
|
Ndugu Kinana
akishiriki kuweka mawe sehemu korofi,angalau kusaidia Lori hilo pichani
lililolala ndani ya msitu huo kwa siku mbili,wapite nae msafara wake uweze
kuendelea na safari.
|
![]() |
|
Ndugu Kinana
akizungumza na baadhi ya Wanahabari aliokuwa ameambatana nao kwenye msafara
wake,baada ya magari kunasa kutokana tatizo la barabara.
|
![]() |
|
Pichani
kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akiongoza kuvuka sehemu korofi ya
barabara kwa miguu,huku madereva wakipiga hesabu zao namna ya kupita.
|
![]() |
|
Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana (alinaerusha jiwe) akishiriki kuziba sehemu korofi kwa
mawe,ili msafara uweze kupita.
|
![]() |
|
Mchuma
ukipita sehemu korofi ya barabara kwa mbinde.
|
![]() |
|
Kila
mmoja akipumua kivyake,baada ya kuvuka salama sehemu korofi ya barabara…
Picha
na Michuzi Jr-Michuzi Media Group-Nkasi-RUKWA.
|















No comments:
Post a Comment