Taharuki ya aina yake ilitokea jana (April 02,2014) eneo la Tabata Relini kwenye yadi ya malori ya Kampuni ya Oilcom baada ya kutokea kishindo kikubwa kilichotokana na kupasuka kwa tanki la mafuta.
Tukio hilo
lililotokea saa 11 jioni, lilizua hofu miongoni mwa wakazi na wafanyakazi wa
eneo hilo, na lilitokana na hitilafu ya kiufundi wakati wa kulitengeneza tanki
hilo.
Mashuhuda wa
tukio hilo lililojeruhi watu watatu waliliambia Mwananchi kuwa mlipuko huo
ulitokea wakati fundi akichomea sehemu ya tanki katika karakana ya magari ya
kampuni hiyo.
“Kuna fundi
alikuwa juu ya lori akipima mifuniko na chini alikuwepo dereva wa lori hilo na
fundi mwingine wa kuchomea vyuma akichomea, wote walikuwa wakiendelea na kazi.
“Dereva wa
lori hilo alikuwa akimuelekeza fundi sehemu ya kuchomea na ghafla ukatokea
mlipuko mkubwa,” alisema Omari Wenge, fundi katika karakana hiyo.
Alisema
mlipuko huo ulimtupa chini fundi aliyekuwa juu ya tanki na kulikosababisha
aumie usoni na sehemu za kifuani.
Shuhuda huyo
alisema dereva na fundi wa kuchomea, waliumizwa sehemu mbalimbali za mwili kwa
kupigwa na vipande vya mabati ya tanki na kichwa cha gari hilo.
Majeruhi wa
ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Camillus Wambura alisema kuwa hakuwa
amepata taarifa zozote za ajali hiyo hivyo angetujulisha pindi angezipata.
Mwandishi wa
habari hizi alishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa karakana hiyo wakipewa huduma
ya kwanza baada ya kuzimia kwa mshtuko huku wengine wakiweweseka kwa hofu.
Kichwa cha
lori hilo kilichakazwa na mlipuko huo ambao moja ya mabati yanayoligawa tanki
hilo yalitupwa upande wa pili wa Barabara ya Mandela.
Sehemu ya
juu ya mbele ya lori hilo, ilitupwa juu ya paa la moja ya majengo ya karakana
hiyo huku chini zikiwa zimetapakaa nyaraka na mabaki mengine ya sehemu ya mbele
ya lori hilo.
Naye mmoja
wa mashuhuda, Boniface Msisi aliyekuwemo ndani ya karakana hiyo, alisema hali
ndani ya eneo hilo ilibadilika ghafla huku kila mfanyakazi akitafuta mlango wa
kutokea.
Aidha lori hilo lilikuwa limetoka safari
hivyo walikuwa wakilifanyia matengenezo ya kawaida.
Juhudi za
kuupata uongozi wa karakana kuzungumzia ajali hiyo uligonga mwamba kutokana na
viongozi hao kuwa katika harakati za kuokoa maisha ya majeruhi.
Habari
Na:-Mwananchi.






No comments:
Post a Comment