UEFA 2013/2014:-Haya ndio matokeo Chelsea ikibondwa 3-1 na PSG huku C.Ronaldo akiikamata rekodi ya L.Messi,Real Madrid ikishinda 3-0 dhidi ya Borussia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 03, 2014

UEFA 2013/2014:-Haya ndio matokeo Chelsea ikibondwa 3-1 na PSG huku C.Ronaldo akiikamata rekodi ya L.Messi,Real Madrid ikishinda 3-0 dhidi ya Borussia.


Beki David Luiz akimtungua kipa wake mwenyewe Petr Cech kuipatia PSG bao baada ya Ezequiel Lavezzi kupiga Frikiki safi ambayo Kipa Petr Cech alishindwa kuzuia na kumparaza Zlatan Ibrahimovic kisha Mchezaji wa Chelsea David Luiz kuusindikiza wavuni na kufungwa na PSG 3-1-April02,2014.
Chelsea imeanza vibaya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuchapwa mabao 3-1 na wenyeji wake PSG usiku huu April 02,2014,Katika mechi iliyopigwa huko Ufaransa kwa wenyeji kupata bao katika dakika ya 4 tu ya mchezo kupitia kwa Ezequiel Lavezzi, lakini Chelsea wakasawazisha katika dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalty kupitia Eden Hazard baada ya Oscar kuangushwa.

Chelsea walisawazisha kwa Penati ya Dakika ya 27 iliyopigwa na Eden Hazard na ilitolewa na Refa Milorad Mazic kutoka Serbia alipoamua Sentahafu wa PSG Thiago Silva ‘kamwangusha’ Oscar.

Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 1-1.

PSG walifunga Bao lao la 2 baada ya Ezequiel Lavezzi kupiga Frikiki safi ambayo Kipa Petr Cech alishindwa kuzuia na kumparaza Zlatan Ibrahimovic kisha Mchezaji wa Chelsea David Luiz kuusindikiza wavuni.

Nchezaji alietoka Benchi, Javier Pastore, aliipa PSG Bao la 3 katika Dakika ya 90 baada ya kupokea Mpira wa kurushwa na kuwatoka Cesar Azpilicueta, Frank Lampard na John Terry kisha kupiga Shuti la chini chini na kumshinda Kipa Petr Cech.

Timu hizi zitarudiana huko Stamford Bridge Jumanne Aprili 8.
 
 Oscar wa Chelsea akiangushwa na Thiago Silva wa PSG na  Chelsea peneti ilitolewa na Refa Milorad Mazic kutoka Serbia .

Mategemeo ya Chelsea ni katika mechi ya pili ambayo itapigwa mjini London na ili isonge inatakiwa kushinda kuanzia mabao 2-0.

Kipindi cha pili, PSG walifunga mabao mawili wakianza na dakika ya 61 baada ya beki David Luiz kujifunga kutokana na mpira wa krosi kabla ya Javier Pastore kuwachambua mabeki wa Chelsea na kuandika bao la tatu katika dakika ya 90 ya mchezo huo.

Real Madrid imebisha hodi Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Borrusia Dortmund usiku huu wa (April 02,2014) kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu katika Robo Fainali ya kwanza ya michuano hiyo.
Katika Dakika ya 57, Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, alipiga Bao la 3 baada kumtoka Kipa Roman Weidenfeller kufuatia kupokea pasi safi ya Luka Modric.

Ronaldo hakumaliza Mechi hii baada ya kuumia na kutolewa nje katika Dakika ya 80 ya mchezo.

Katika mchezo mwingine wa Robo fainali, Real Madrid, wakicheza Uwanjan kwao Santiago Bernabeu Jijini Madrid Nchini Hispania, Usiku wa April 02,2014,wameichapa Borussia Dortmund Bao 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Gareth Bale ndie aliefunga Bao la Kwanza katika Dakika ya 3 tu baada kuunganisha pasi safi ya Daniel Carvajal na kumzidi akili Kipa Roman Weidenfeller.

Bao la Pili la Real lilifungwa katika Dakika ya 27 kupitia Isco kwa Shuti la chini toka Mita 20 ambapo Katika Dakika ya 57, Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, alipiga Bao la 3 baada kumtoka Kipa Roman Weidenfeller kufuatia kupokea pasi safi ya Luka Modric.

Hilo ni Bao la 14 kwa Ronaldo kwenye Ligi ya Mabingwa Msimu huu wa 2013/2014 na ameifikia Rekodi ya Lionel Messi aliefunga Bao 14 katika Mechi 11 za UEFA Msimu wa 2011/12 wakati Ronaldo amechukua Mechi 8 tu.

Timu hizi zitarudiana huko Signal Iduna Park, Jijini Dortmund, Germany Jumanne Aprili 8.



UEFA 2013/2014 ROBO FAINALI.


Marudiano

[Saa 3 Dak 45 Usiku]

[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]

Jumanne Aprili 8,2014.

Chelsea v Paris Saint-Germain [1-3]
Borussia Dortmund v Real Madrid [0-3]

Jumatano Aprili 9,2014.

Bayern Munich v Manchester United [1-1]
Atletico Madrid v Barcelona [1-1]

-DROO YA NUSU FAINALI: 11 Aprili,2014.

-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili,2014.

-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad