VPL 2013/2014:-Yanga SC sasa na matumaini ya Kutetea Ubingwa wa Ligi kuu Bara baada ya kushinda 5-1 dhidi ya JKT Ruvu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 06, 2014

VPL 2013/2014:-Yanga SC sasa na matumaini ya Kutetea Ubingwa wa Ligi kuu Bara baada ya kushinda 5-1 dhidi ya JKT Ruvu.


Mfungaji wa mabao matatu ya Yanga SC katika ushindi wa 5-1 dhidi ya JKT Ruvu, Mrisho Ngassa wa pili kulia akishangilia na wenzake jioni hii (April 6, 2014, katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara,Yanga SC imezinduka na kufufua matumani ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.

Ushindi huo, unaifanya Yanga SC inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kutimiza pointi 49 baada ya kucheza mechi 23 sawa na Azam FC inayoongoza ligi hiyo kwa pointi zake 53. Mbeya City ni ya tatu kwa pointi zake 46 baada ya kucheza mechi 24.

Yanga leo(April 06,2014) ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0, Mrisho Ngassa akifunga la kwanza dakika ya tisa akimalizia pasi nzuri ya Mrundi Didier Kavumbangu ndani ya boksi.

Ngassa kafunga mabao 3 katika mchezo huo na kufikisha mabao 11 katika Ligi Kuu msimu huu wa 2013/2014 huku magoli mengine ya Yanga SC yamefungwa na Hussein Javu na Didier Kavumbagu nao walipiga mabao mengine mawili yaliyoiongezea Yanga akiba hiyo nzuri ya mabao hadi kufikisha matano.

Bao la kufutia machozi la JKT Ruvu inayofundishwa na kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga SC , Freddy Felix Minziro lilifungwa na Nashon Naftali dakika ya 83 akimalizia krosi ya Damas Makwaya. 

AIDHA –Kwenye Mechi mbili pekee za  Ligi Kuu Vodacom jana April 05,2014, zilizochezwa, Kagera Sugar na Simba SC zilitoka Sare ya Bao 1-1 huko Kaitaba, Mjini Bukoba na huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Ashanti United ilitoka 0-0 na Mbeya City.

Ligi hiyo itaendelea hapo April 09,2014  kwa Ruvu Shooting kuwakaribisha Vinara wa ligi Azam FC.

Jumatano Aprili 9,2014.

Ruvu Shooting v Azam FC

MSIMAMO VPL 2013/2014.


NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
23
15
8
0
31
53
2
Yanga SC
23
14
7
2
40
49
3
Mbeya City
24
12
10
2
13
46
4
Simba SC
24
9
10
5
15
37
5
Kagera Sugar
23
8
10
5
3
34
6
Mtibwa Sugar
22
7
8
7
1
29
7
Coastal Union
23
6
11
6
0
29
8
Ruvu Shooting
21
7
8
6
-4
29
9
JKT Ruvu
24
9
1
14
-17
28
10
Ashanti United
23
5
7
11
-17
22
11
Mgambo JKT
22
5
6
11
-18
21
12
Prisons FC
22
3
10
9
-10
19
13
JKT Oljoro
23
2
9
12
-18
15
14
Rhino Rangers
23
2
7
14
-19
13

**MSIMAMO HUU SI RASMI TOKA TFF 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad