EPL 2013/2014:-Arsenal yakung'utwa mabao 3-0 na Everton Uwanja wa Goodison Park na kuzidi kujitoa kwenye mbio za Ubingwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 06, 2014

EPL 2013/2014:-Arsenal yakung'utwa mabao 3-0 na Everton Uwanja wa Goodison Park na kuzidi kujitoa kwenye mbio za Ubingwa.


Mchezaji Romelu Lukaku amefunga katika ushindi wa Everton wa 3-0 dhidi ya Arsenal leo(April 06,2014)katika mchezo wa Ligi kuu soka Nchini Uingereza.


Wakicheza Ugenini huko Goodison Park dhidi ya Everton ambayo inahangaika kuing’oa Nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Uingereza, Arsenal Leo (April 06,2014) hii wametandikwa Bao 3-0 na, pengine, kufuta kabisa matumaini yao ya Ubingwa na pia kuleta wasiwasi mkubwa kama watamudu kumaliza kwenye 4 Bora ili wacheze Mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu Ujao.

Kipigo hiki kimeifanya Arsenal ibakie Nafasi ya 4 ikiwa imecheza Mechi 33 na ina Pointi 64 lakini ushindi kwa Everton, ambao wako Nafasi ya 5, umewafanya waikaribie mno Arsenal na wao sasa wamecheza Mechi 32 na wana Pointi 63.

Everton walipata Bao la Kwanza katika Dakika ya 14 wakati krosi ya Leighton Baines ilipomkuta Romelu Lukaku ambae Shuti lake likaokolewa na Kipa Wojciech Szczesny na kumfikia Steven Naismith aliefunga.

Kwenye Dakika ya 34, Romelu Lukaku alifunga Bao la Pili baada kukokota Mpira toka kulia na kuwaacha Nacho Monreal na Thomas Vermaelen na kufunga kwa Guu la Kushoto.

Bao la Tatu la Everton ni la kujifunga mwenyewe Mikel Arteta katika Dakika ya 62 wakati Kevin Mirallas alipompora Bacary Sagna Mpira na kumpa Steven Naismith ambae alishindwa kumpita Kipa Wojciech Szczesny na Mpira kugombewa na Mirallas na Mikel Arteta na hatimae Arteta kujifunga.

RATIBA MECHI ZIJAZO EPL 2013/2014.

Jumatatu 7 Aprili 2014

2200 Tottenham v Sunderland

Jumamosi 12 Aprili 2014

1700 Crystal Palace v Aston Villa
1700 Fulham v Norwich
1700 Southampton v Cardiff
1700 Stoke v Newcastle
1700 Sunderland v Everton
1700 West Brom v Tottenham

Jumapili 13 Aprili 2014

1530 Liverpool v Man City
1800 Swansea v Chelsea

Jumanne 15 Aprili 2014

2145 Arsenal v West Ham

Jumatano 16 Aprili 2014

2145 Everton v Crystal Palace
2145 Man City v Sunderland


Bottom of Form
Sat 5 Apr 2014 - Premier League 2013/2014.

Man City 4 - 1 Southampton
Aston Villa 1 - 2 Fulham
Cardiff 0 - 3 Crystal Palace
Hull 1 - 0 Swansea
Newcastle 0 - 4 Man Utd
Norwich 0 - 1 West Brom
Chelsea 3 - 0 Stoke
Everton 3 - 0 Arsenal  
West Ham 1 - 2 Liverpool

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad