VPL 2013/2014:-Simba SC v/s Yanga SC katika Picha April 19,2014-Uwana wa Taifa na kutoka sare ya 1-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 20, 2014

VPL 2013/2014:-Simba SC v/s Yanga SC katika Picha April 19,2014-Uwana wa Taifa na kutoka sare ya 1-1.


Mshambuliaji wa Yanga SC, Hamisi Kiiza akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana (April 19,2014) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.


Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza mfungaji wa bao lao la kuongoza, Haroun Chanongo aliyevua jezi huku akifuta machozi ya kilio cha furaha.


Picha juu na chini ni Mashabiki wa Simba SC wakishangilia timu yao jana April 19,2014 ilipocheza na Yanga SC na kutoka sare ya bao 1-1.



Mfungaji wa bao la kusawazisha la Yanga SC, Simon Msuva kushoto akishangilia na wenzake.

Mashabiki wa Yanga SC wakishangilia timu yao jana April 19,2014katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam ilipocheza na Simba SC.

Haya ni baadhi ya Matukio yaliyojitokeza katika mchezo huo wa watani wa jadi Simba na Yanga wa kukamilisha msimu wa Ligi kuu 2013/2014 jana April 19,2014 na kutoka sare ya bao 1-1.



Beki wa Simba SC, Mganda Joseph Owino kushoto akipiga kichwa dhidi ya mshambuliaji wa Yanga SC, Didier Kavumbangu.


Kocha wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.


Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm akiwatazama vijana wake.


Wachezaji wa Yanga SC baada ya kukabidhiwa Medali za ushindi wa pili Ligi Kuu iliyofikia tamati jana (April 19,2014) kwa Azam FC kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ya Vodacom Tanzania bara 2013/2014.


Kikosi cha Yanga SC jana-April 19,2014 dhidi ya Simba SC.


Kikosi cha Simba SC jana-April 19,2014 dhidi ya Yanga SC.Picha Na:-Bin Zuberi.

LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA 2013/2014.

Imefikia tamati (April 19,2014) kwa Mabingwa Azam FC kukabidhiwa Kombe lao huko Azam Complex, Chamazi mara baada ya Mechi yao ya kukamilisha Ratiba ambayo waliifunga JKT Ruvu Bao 1-0.

Kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam, Watani wa Jadi, Yanga na Simba nao walikutana kwenye Dabi ya Kariakoo, isiyokuwa na maana yeyote mbali ya kukamilisha Ratiba, na kutoka Sare ya Bao 1-1.

Kwenye Mechi hiyo, iliyohudhuriwa na Watazamaji wachache tofauti na desturi, Simba walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 76 Mfungaji akiwa Haruna Chanongo na Yanga kusawazisha kwa Bao la Dakika ya 86 la Simon Msuva.

Mechi pekee iliyokuwa na umuhimu mkubwa ni ile iliyochezwa Uwanja wa Jamhri huko Morogoro kati ya Tanzania Prisons na Ashanti United na Prisons kuifunga Ashanti Bao 1-0 na wao kupona na kuishusha Daraja Ashanti ambao wanaungana na JKT Oljoro na Rhino Rangers kuporomoka Daraja.

VPL, LIGI KUU VODACOM 2013/2014.

Mechi za mwisho za Ligi-Jumamosi Aprili 19,2014.

Mbeya City 1 Mgambo JKT 0 [Sokoine, Mbeya]

Tanzania Prisons 1 Ashanti United 0 [Jamhuri, Morogoro]

JKT Ruvu 0 Azam FC [Azam 1 Complex, Chamazi]

JKT Oljoro 1 Mtibwa Sugar 1 [Sheikh Amri Abeid, Arusha]

Coastal Union 0 Kagera Sugar 1 [Mkwakwani, Tanga]

Yanga 1 Simba 1 [National Stadium, Dar es Salaam]

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad