Akizungumza jana (April 18,2014), Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene
alisema gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu.
Alisema mbali na kujieleza, gazeti hilo limepewa siku saba hadi Aprili
23, mwaka huu, kukanusha taarifa hiyo.
![]() |
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ,
akiowaonesha
waandishi wa habari ,
hati halisi
ya Muungano ikulu jijini Dar es Salaam
(April
14,2014).
|
Kwa mujibu wa Mwambene, katika gazeti hilo toleo na 0091 la Aprili 17-23,
mwaka huu lenye kichwa cha habari ‘Hati za Muungano utata’, taarifa
husika inakebehi hati hiyo na kujenga taswira kwamba ni ya kughushi na batili.
Linadai waandishi wawili ndiyo waliona kati ya waandishi zaidi ya 20
waliokuwepo kwenye mkutano wa Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
"Taarifa ya gazeti la Mawio ni ya kimawazo na imeandikwa pasipo
shaka kutimiza malengo na maslahi binafsi wanayojua,” alisema.
Alisema pamoja na maelezo ya Katibu Kiongozi, Sefue, gazeti hilo liliamua
kwa utashi wake kukejeli na kuuaminisha umma wa Watanzana kwamba Hati ya
Muungano ina utata.
![]() |
Hii ni sehemu ya Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar...1964.
|
No comments:
Post a Comment