![]() |
Wachezaji wa
Azam FC wakiongozwa na nahodha wa timu hiyo John Boko wakati wa kupokea Kombe
la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Vodacom Tanzania Bara msimu wa mwaka 2013/2014.
|
Wachezaji wa
Azam FC wakishangilia.
|
![]() |
Wachezaji na
mashabiki wakishangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara 2013/2014.
|
![]() |
Nahodha wa Azam FC, John Boko akiwa ameshika
Kombe la Ubingwa wa Ligi ya Soka Tanzania Bara-2013/2014.
|
Mabingwa
wapya wa Tanzania Bara, Azam FC wamekabidhiwa rasmi kombe lao jana (April
19,2014)na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Kombe hilo
limekabidhiwa baada ya Azam FC kukipiga na JKT Ruvu na kuichapa timu hiyo ya
jeshi kwa mabao 1-0 ambayo imeteremka daraja.
Bryan
Umonyi, raia wa Uganda ndiye alifunga bao hilo baada ya kuingia kuchukua nafasi
ya Kipre Tchetche.
Hadi
wanakabidhiwa kombe, mechi hiyo ilikuwa imejaza watu wengi na mashabiki wakiwa
wengi kwa kuwa pambano hilo halikuwa na kiingilio.
Lakini pia
kulikuwa na shoo kutoka kwa vikundi mbalimbali wakiwemo Wanaume TMK
walioongozwa na Mheshimiwa Temba.
Kikosi cha Rhino ya Tabora 2013/2014. |
Aidha kumalizika
kwa Ligi hiyo VPL 2013/2014-April 19,2014:-Ni rasimi sasa Rhino ya Tabora,
Ashanti United na JKT Oljoro rasmi wameteremka daraja na kurejea Ligi Daraja la
Kwanza.
Ashanti
imeshuka baada ya kuchapwa bao 1-0 na Prisons ya Mbeya katika mechi iliyochezwa
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, April 19,2014.
Wachezaji wa
Ashanti United, walilia kwa uchungu wakionyesha kutofurahia kuteremka daraja.
Rhino nao
wakiwa nyumbani Tabora, jana wamepigwa mabao 2-0 na Ruvu Shooting kwa magoli ya
Hamis Mohammed na Elias Maguri ndiyo yaliyoimaliza timu hiyo ya Tabora.
Kikosi cha JKT Oljoro 2013/2014. |
Mjini
Arusha, JKT Oljoro wameteremka rasmi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya
Mtibwa Sugar.
Timu hiyo ya
jeshi inakuwa timu ya tatu kuteremka daraja.
Kutokana na
kuteremka kwa timu hizo, Ndanda FC, Stand ya Shinyanga na Polisi ya Morogoro
ndiyo wamepanda rasmi Ligi Kuu Bara msimu ujao wa 2014/2015.
Kikosi cha Ashanti United 2013/2014. |
MSIMAMO WA LIGI VODACOM TANZANIA BARA 2013/2014.
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Azam FC | 26 | 18 | 8 | 0 | 51 | 15 | 36 | 62 |
2 | Young Africans | 26 | 16 | 8 | 2 | 61 | 19 | 42 | 56 |
3 | Mbeya City | 26 | 13 | 10 | 3 | 33 | 20 | 13 | 49 |
4 | Simba SC | 26 | 9 | 11 | 6 | 41 | 27 | 14 | 38 |
5 | Kagera Sugar | 26 | 9 | 11 | 6 | 23 | 20 | 3 | 38 |
6 | Ruvu Shooting | 25 | 9 | 8 | 8 | 26 | 32 | -6 | 35 |
7 | Mtibwa Sugar | 26 | 7 | 10 | 9 | 30 | 31 | -1 | 31 |
8 | JKT Ruvu | 26 | 10 | 1 | 15 | 23 | 40 | -17 | 31 |
9 | Coastal Union | 26 | 6 | 11 | 9 | 17 | 20 | -3 | 29 |
10 | Mgambo JKT | 26 | 6 | 8 | 12 | 18 | 35 | -17 | 26 |
11 | Tanzania Prisons | 26 | 6 | 10 | 10 | 26 | 33 | -7 | 28 |
12 | Ashanti United | 26 | 6 | 7 | 13 | 20 | 39 | -19 | 25 |
13 | JKT Oljoro | 26 | 3 | 10 | 13 | 19 | 37 | -18 | 19 |
14 | Rhino Rangers | 25 | 3 | 7 | 15 | 18 | 37 | -19 | 16 |
No comments:
Post a Comment