Akiiwasilisha
ripoti hiyo, Mwakilishi wa IMF nchini, Thomas Baunsgaad, alisema licha ya
uchumi huo kukua, lakini haujaweza kupunguza umasikini.
Alisema kwa Tanzania, gharama za mikopo kutoka nje imekuwa ni mikubwa na inaongezeka mwaka hadi mwaka na ndiyo sababu inayosabaisha hali ya umasikini kwa wananchi.
Imeeleza kuwa Tanzania kasi ya ukopaji imeongezeka kutoka asilimia 28 ya pato la taifa hadi asilimia 42 ya pato la taifa kwa mwaka huu.

Kadhalika,
ripoti hiyo imeeleza kuwa katika nchi za Afrika ili kuondokana na umasikini,
lazima kuwepo na sera ambazo zitaweka kupunguza umaskini.
Baadhi ya sera hizo ni pamoja na kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa zaidi, kuongeza idadi ya viwanda vitakavyoongeza ajira, kuwekeza katika ukuaji na upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi, pamoja na kuboresha mazingira ya kufanya biashara.
Pia ripoti hiyo ilibaini uwapo wa matumizi makubwa ya fedha kwa serikali kuliko mapato inayoingiza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji kutoka Repoa, Profesa Samwel Wangwe, alisema ili kupunguza hali ya umasikini nchini uendane na ukuaji wa uchumi, serikali inapaswa kupunguza matumizi makubwa ya fedha.

Source:-Nipashe.

No comments:
Post a Comment