Aliyekua
Mwenyekiti wa tume ya taifa ya kukusanya maoni ya katiba Mheshimiwa Jaji Joseph
Sinde Warioba leo kupitia kipindi cha dakika 45 cha ITV amezungumza mambo mengi
sana ya msingi kuhusu muungano yakiwemo yale yanayoihusu Tanzania bara na
Tanzania visiwani,haya ni miongoni mwa mambo hayo.
1:-.Mchakato
umeanza nadhani kwa kusuasua bunge limechukua muda mrefu kutengeneza kanuni na
wameanza haikua mwanzo mzuri mpaka imefika mahali wamefarakana lakini
tunaendelea na mchakato bado matumaini yapo.
2:-.Sisi
tulipoenda kufanya kazi tulienda kukusanya maoni ya Wananchi tulichukua maoni
ya Wananchi kwa ujumla tukapeleka mapendekezo ambayo tuliamini ni ya
kuwaunganisha Wananchi tulichotegemea ni kwamba Bunge nalo lingekwenda na
muelekeo huo lakini toka mwanzo likaonekana bunge limejiunda katika makundi
badala ya kuanagalia suala lenyewe la maoni ya Wananchi likaanza kuonekana
mgawanyiko toka mwanzo wanatengeneza kanuni.
3:-.Wakati
tunakabidhi rasimu ya kwanza nilisema ili tuendelee na muungano inahitaji
ukarabati mkubwa na tukasema kwa tathmini ya tume itakua ni vigumu sana kufanya
ukarabati huo ndiyo maana tumependekeza serikali tatu.
4:-.Tulipopita
kwa wananchi walikua wanauzungumzia muungano walisema tuuboreshe muungano
lakini wakati wote wakasema tatizo letu ni muundo wengi walizungumzia muundo
tulionao,tulianza kuorodhesha mambo yote yaliyosemwa na bara na visiwani.
5:-.Zanzibar
wamekwenda wamepitisha sheria wanasema sheria zozote zitakazotungwa na Bunge la
Muungano haziwezi kutumika Zanzibar mpaka zipelekwe kwenye Baraza la
Wawakilishi maana yake Baraza la wawakilishi limekua kubwa kuliko Bunge la
Muungano.
6:-.Tuna
mahakama ya rufaa ina madaraka nchi nzima wameenda wametunga wamebadili katiba
yao wamesema kuna mambo fulani fulani haki za binadamu,mashauriano yanayotoka
kwenye mahakama za kazi na kutafsiri katiba ya Zanziba hayo hayatakuwa kwenye
madaraka ya muungano lakini kwenye katiba ya muungano imesema katiba hii ina
mamlaka yote.
7:-.Tusiingize
jeshi kwenye mambo ya siasa za makundi Jeshi ni la nchi,mimi nimetumikia nchi
hii nimekua kwenye utumishi wa umma kwa muda mrefu mpaka nikawa Waziri Mkuu na
nilipokuwa Waziri Mkuu nilikua nazunguka nchini kuangalia shughuli za
kimaendeleo na kila nilipoenda kama kuna kambi ya jeshi karibu nilikua naenda
kukaa nao.






No comments:
Post a Comment