AJALI:-Watu 14 wafariki katika Ajali mkoani Singida-April 28,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 29, 2014

AJALI:-Watu 14 wafariki katika Ajali mkoani Singida-April 28,2014.


Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.Picha Na Maktaba .

Watu 13 aiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kwenda Dar es Salaam katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku wa jana April 28,2014.

Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo hilo.

Basi hilo lililokuwa likitokea mkoani Kigoma kwenda jijini Dar es Salaam halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida.

Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad