Kamanda wa
polisi mkoani Simiyu, Charles Mkumbo alisema ofisini kwake mjini hapa jana kuwa
tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nane za usiku wakati mtuhumiwa Baya
Seni (30) akiwa amelala na familia yake kijijini hapo, ndipo alipokurupuka
ndani akampiga mtoto wake Amos Baya (3) na kisha kumtupa na kumtelekeza nje ya
nyumba.
Alisema,
Seni katika maelezo yake kituo cha polisi alisema alifikia uamuzi huo kwa kuwa
hakuona thamani ya mtoto wa kiume kwenye familia yake kwani uzoefu umeonesha
kuwa watoto wa kiume wakikua hudai kupata mirathi kutoka kwa wazazi wao .
Alisema
kinyume chake watoto wa jinsia ya kike wakikua watamuongezea utajiri wa mifugo
atakapolipwa mahari ili waolewe na baada ya kuolewa hawawi mzigo tena kwenye
familia yake bali mzigo huo huhamia kwenye familia atakayoolewa. Mtoto huyo
aliokolewa na majirani baada ya kusikia kilio.
Mama wa
mtoto huyo Elizabeth Paulo alisema, mume wake alikuwa akimtesa sana mtoto wake
akimbagua kwa vile yeye ni wa jinsia ya kiume na kwamba hana faida kwake.
Habari
Na:-Shangwe Thani- Simiyu
No comments:
Post a Comment