![]() |
Chelsea imeshinda kwa mabao 2-0, yakiwa yamefungwa na Andre Schurrle na
Demba Ba.
|
![]() |
Ikiwa nyumbani,Chelsea imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini na
kuiondoa PSG ya Ufaransa baada ya mechi
ya kwanza, Chelsea ilipoteza kwa mabao 3-1, hivyo ilihitaji mabao mawili tu
kusonga mbele.
|
Kocha Jose Mourinho ambaye timu yake ilifungwa 3-1 katika mchezo wa
kwanza mjini Paris, Ufaransa alipagawa kwa furaha baada ya bao la Ba akaenda
kushangilia na wachezaji wake kwenye kibendera.
Mabao ya Marco Reus dakika ya 24 na 37 yaliwafanya wenyeji waende
kupumzika wanaongoza kwa 2-0 na kufanya matokeo ya jumla yawe 3-2 baada ya
kufungwa 3-0 katika mchezo wa kwanza.
CLUB
ATLÉTICO DE MADRID v FC BARCELONA
-Estadio
Vicente Calderon, Madrid, Nyumbani kwa Atlético Madrid, Atletico hawajawahi kuwafunga FC Barcelona
tangu Februari 2010 ambapo Diego Forlán na Simão walipiga Bao na kuwapa ushindi
wa Bao 2-1.
Tangu wakati
huo, Barcelona hawajafungwa katika Mechi 5 walizocheza Nyumbani kwa Atletico na
mara ya mwisho kushinda ni Mei Mwaka Jana waliposhinda 2-1.
Msimu huu,
Atletico na Barca zimeshakutana mara 4 na mara zote kutoka Sare lakini safari hii
ni lazima Barca washinde au kupata Sare yoyote ya kuanzia Bao 2-2 ili wasonge
mbele.
FC BAYERN
MÜNCHEN v MANCHESTER UNITED FC
-Allianz
Arena, Munich,Bayern
wanatinga kwenye Mechi hi wakiwa wameshindwa kuzifunga Klabu za England katika
Mechi zao 4 zilizopita.
Wayne
Rooney anena:-
“Kila Mtu
kila Mwaka huwa na Timu anayoona ndio itakuwa Bingwa-kama vile Barca na
Bayern-lakini Siku zote halitokei hilo! Wakati Chelsea walipotwaa Ubingwa 2012,
mara 3 walikaribia kutolewa! Tunaamini tutasonga! Tuna Wachezaji wazuri wa
kufanya hilo!”
Bayern,
ambao ni Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, ili kusonga mbele wanahitaji Sare ya
0-0 au ushindi lakini Sare ya Bao 2-2 na kuendelea itawapa ushindi Man United
kwa Bao za Ugenini.
Jumatano
Aprili 9,2014.
Bayern
Munich v Manchester United [1-1]
Atletico
Madrid v Barcelona [1-1]
No comments:
Post a Comment