![]() |
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma David A. Misime - SACP akiongea na wanahabari leo April 17,2014.
|
Jeshi la
Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu watatu kwa kosa la Kupatikana na
Bhangi kiasi cha Kilogramu 133.5 yenye thamani ya Ths. 20,025,000/= bei ya
mitaani (street value). Watuhumiwa hao wamekamatwa mnamo tarehe
16/04/2014 majira ya 7:30 mchana eneo la Stend Kuu ya mabasi katika Manispaa na
Mkoa wa Dodoma.
![]() |
Watuhumiwa hao waliokamatwa. |
Watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha Bhangi katika mabegi
baada ya kupanda basi kutokea Kijiji cha MANONGA – TINDE Mkoani SHINYANGA
kwenda jijini Dar es Salaam katika basi namba No. T.931 CGU mali ya kampuni ya NEW
FORCE linalofanya safari zake kutokea Kahama kwenda jijini Dar es Salaam.
Watu
hao walifahamika kwa majina ya:-
1.
CALVIN S/O PROSPER SALEKA, miaka 23, kabila Mchaga, Mwanafunzi wa chuo cha
Institute of Finance Management (IFM) cha Dar es Salaam, mwaka wa pili,
alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 51kgs
2.
JOHN S/O JOSEPH, Miaka 31, kabila msukuma, mkulima na mkazi wa Kinondoni Dar es
Salaam, alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito wa 42.5kgs.
3.
JOSEPH S/O CHARLES BATONI, Miaka 22, kabila msukuma, mkulima na mkazi wa
Shinyanga. alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 36.5kgs
Watuhumiwa
hao walikamatwa kufuatia taarifa za raia mwema aliyewatilia mashaka na kutoa
taarifa Polisi.
![]() |
Basi namba
No. T.931 CGU ,
mali ya
kampuni ya NEW FORCE
|
Mbinu waliyotumia kusafirisha ni kuhifadhi katika mabegi
makubwa ya nguo na kufunga kwa mifuko ya nailoni kisha kusaga vitunguu na
kuweka katika mabegi hayo pamoja na kupulizia manukato (perfume) ili kuondoa
harufu wasiweze kugundulika kirahisi.
Tukio
lingine katika kijiji cha Central Kiteto Tarafa ya Mlali Wilaya ya Kongwa
zilikamatwa lita 300 za Pombe haramu ya Gongo nyumani kwa Salumu s/o Chamagulu
ambaye alikimbia baada ya kuona Polisi na tunaendelea kumtafuta.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David A. Misime –
SACP, anawapongeza kwa dhati raia wema wanaoshirikiana na Jeshi la Polisi kwa
kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuendelea kudhibiti madawa ya kulevya
na Pombe ya Moshi inayoharibu vijana wengi.
No comments:
Post a Comment