PICHA:-Taswira toka Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma April 17, 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 18, 2014

PICHA:-Taswira toka Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma April 17, 2014.


 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu Mhe.Samia Suluhu akiwa anafuatilia mchango wa Mhe.William Lukuvi kwa makini ambapo Bunge hilo maalum la Katiba Jana (April 17, 2014) Limeendelea na mjadala wa rasimu ya katiba huku wajumbe wanaounda Umoja wa UKAWA wakiendelea kususia mjadala huo.

Hali ya hewa yarejea kuwa ya kawaida bunge maalum la katiba mjini Dodoma Jana (April 17,2014).


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, William Lukuvi akichangia Bungeni Mjini  Dodoma  jana (April 17,2014) .......ambapo Waziri Lukuvi, amelazimika kusitisha safari yake ya kimatibabu nchini India, kwa ajili ya kufafanua madai ya wajumbe wa UKAWA kuwa amewatisha wananchi akiwataka kutokubali muundo wa serikali tatu, vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa serikali ya muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.”

Bunge maalum la Katiba Jana (April 17,2014) limeendelea na mjadala wa rasimu ya katiba huku wajumbe wanaounda Umoja wa UKAWA wakiendelea kususia mjadala huo baada ya Mwenyekiti wa Bunge hilo Bw Samuel Sitta kubainisha kuwa Bunge hilo haliwezi  kusitisha mjadala kutokana na kutokuwepo wajumbe hao, kwani akidi ya Wajumbe waliopo inatosha kuendelea na mjadala kulingana na kanuni za Bunge hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad