![]() |
Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ndege baada ya kuwasili Uwanja wa
Ndege wa Kigoma kuanza ziara ya siku tano mkoani humo jioni hii ya April 08,2014.
|
![]() |
|
![]() |
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wa
mkoa Dk. Kaborou wakati akipita katika paredi la UVCCM alipopokelewa Uwanja wa
Ndege wa Kigoma jioni ya leo.
|
![]() |
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa
Kigoma,Kanali Mstaafu Issa Machibya jioni ya leo mara baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Kigoma.
|
![]() |
Kinana
akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog
|
![]() |
Sehemi ya Waendesha boda boda wakiupokea msafara wa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana mapema leo April 08,2014, jioni,mara baada ya kuwasili mjini Kigoma.
|
Akiwa mkoani
Kigoma,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana anaanza ziara ya siku tano
mkoani humo sambamba na ujumbe wake lengo likiwa ni kukagua uhai wa chama pamoja na
kuzindua miradi kadhaa ya kimaendeleo .
Ratiba iliyotolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Mohamed Nyawenga, inaonyesha kuwa, baada ya kutoka Uwanja wa Ndege, Kinana ataenda Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma, ambako atafanya shughuli kadhaa ikiwemo kusaini kitabu cha wageni na kupokea taarifa ya Chama, kuzungumza na Kamati ya Siasa ya mkoa na baadaye kufungua mradi wa maduka.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa, Aprili 9, 2014, Kinana atakwenda wilaya ya Kasulu ambako baada ya kusaini kitabu wilayani na kuzungumza katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya hiyo, atafanya shughuli kadhaa katika Kata mbalimbali.
Kinana anaaza ziara hiyo, baada ya kumaliza nyingine ya siku sita katika mkoa wa Rukwa, ambako katika ziara hiyo alikagua uhai wa chama, utekelezaji wa ilani na Chama na kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia za kuzitatua pale zilizpojitokeza.
Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungmza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM
Mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Kigoma leo-April
08,2014.
|
Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akielezea jinsi CCM ilivyoshinda kwa
kishindo katika chaguzi za Chalinze, Kalenga na madiwani wakati wa mkutano wa
Halmashauri ya Mkoa wa Kigoma.
|
Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma wakisikiliza kwa makini wakati Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza nao leo-April 08,2014, baada ya kupewa taarifa
ya mkoa huo.
|
Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akigalia mawe yanayotumika kujengea mabanda
ya maduka yanayojengwa na CCM Mkoa wa Kigoma.
|
Kinana
akikagua ujenzi wa mabanda ya maduka ambao ni mradi wa CCM Mkoa wa Kigoma.
|
Ndugu,Kinana
akiongozwa na Mchumi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Kadri Mushi kukagua mabanda ya
maduka yanayojengwa na CCM Mkoa wa Kigoma.
|
No comments:
Post a Comment