BREAKING NEWS:-Chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda Kiti cha Ubunge Jimbo la Chalinze kura 20812 dhidi kura 2638 za CHADEMA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 06, 2014

BREAKING NEWS:-Chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda Kiti cha Ubunge Jimbo la Chalinze kura 20812 dhidi kura 2638 za CHADEMA.

Matokeo ya awali kwa baadhi ya vituo yanaonesha kuwa mgombea wa CCM Ridhiwani Kikwete ameshinda kwa asilimia 90.

Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Chalinze yametangazwa Chama cha Mapinduzi CCM kimepata jumla ya kura 20812,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kimepata idadi ya jumla kura 2828 na chama cha Wananchi CUF kimepata kura 474.

Hivyo chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda Kiti cha Ubunge Jimbo la Chalinze
CCM  20812    CDM 2638     CUF 473   AFP 78   NRA 59.

Uchaguzi wa mdogo wa Jimbo la Chalinze umefanyika huku ukigubikwa na kasoro kadhaa, ikiwa ni pamoja na watu wachache kujitokeza vituoni kupiga kura, wapiga kura kulalamika ‘kupokwa’ vitambulisho vyao, vituo kuwa majumbani kwa watu, huku pia kukiwa na hofu ya vurugu.

Aidha Wananchi wa Chalinze walikuwa wakipiga kura mbunge wao, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Said Bwanamdogo aliyefariki mapema mwaka huu.
CHINI ni Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Jimbo la Chalinze yalipoanza kutoka kama ushindani ukiwa kwa CMM na CHADEMA.

KATA YA TALAWANDA

CCM 1192

CDM 104

CUF 4

AFP 7

NRA 1

KATA YA MBWEWE

CCM 331

CHADEMA 72

CUF 14

KATA YA MPAJI

CCM 124

CDM 10

CUF 12

KATA YA KWAMTONGA

CCM 83

CDM 2

CUF 11

NRA 1

AFF 2

 KATA KIBINDU

CCM 1313

CDM 300

 KATA CHANGALIKWA

CCM 203

CDM 25

CUF 3



Aidha kwa matokeo hayo katika Jimbo la Chalinze Chama cha Mapinduzi CCM imeshinda Kata Zote Kwa Asilimia zaidi ya 90.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad