|
Chungu cha
ajabu kilichokutwa juu ya kaburi la mtoto Agnes Mlawa katika makaburi ya
Makanyagio mjini Iringa leo (April 06,2014) kikiwa kinafoka
damu.
|
|
Baada ya
kufunguliwa chungu hicho ndani kulikuwa
na damu, maini na kichwa cha ndege.
|
|
Wananchi
wakishuhudia chungu hicho cha ajabu kilichopo kushoto karibu na jembe.
|
|
Baba wa
mtoto Agnes Mlawa akichimbua chungu hicho.
|
|
Baba wa mtoto huyo kulia akisaidiwa na msamalia
mwema kufungua chungu hicho.
|
|
Msamaria
mwema akionyesha vitu vilivyopo ndani.
|
|
Mzee Mlawa
akiwasha kiberiti kwa ajili ya kuteketeza chungu hicho.
|
|
Chungu
kikiteketezwa kwa moto.
|
|
Wananchi na
mzee Mlawa (kulia) wakitazama tukio la kuteketezwa chungu hicho.
|
Mauzauza
yametokea katika kaburi la mtoto Agnes
Mlawa (8) mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa aliyezikwa mwaka jana baada ya baba wa
mtoto huyo kukuta chungu cha
ajabu chenye damu, maini na kichwa cha ndege kaburini hapo.
Tukio hilo la aina
yake limetokea leo (April 06,2014) majira ya saa
mbili asubuhi katika makaburi ya
Makanyagio mjini Iringa wakati baba
mzazi wa mtoto huyo Bw. Mlawa akichembua
kaburi hilo na mara baada ya
kumaliza ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu cha ajabu kuibuga juu
ya kaburi hilo.
"Mimi
nilikuja hapa kusembua kaburi la mwanangu ila baada ya kumaliza ghafla nilikuta
kama damu zinaruka juu kutoka kaburini
na baada ya kuchunguza ndipo nilipoona chungu hicho kikiibuka juu ya kaburi
"
Alisema kuwa chungu
hicho kilikuwa kimefunikwa na
kitambaa cheusi juu ambacho kililowa dawa na kufungwa kamba ya nguo ya kijani
na kutokana na tukio hilo la ajabu
alilazimika kuacha jembe juu ya kaburi na kukimbia kuita watu wanaopita barabarani ili kuomba msaada.
Mzazi huyo
anadai kuwa mazingira ya kifo cha mtoto
wake yalikuwa ni ya kushangaza baada
ya kuugua kwa muda wa siku nne pekee na kufariki dunia.
Hata hivyo alisema
kwa kuwa kwa upande wake haamini
mambo ya kishirikiana hakuona sababu ya
kumwita mganga wa kienyeji kwa ajili ya kushughulikia zoezi la kuchoma
chungu hicho na badala yake kuamua kuifanya kazi hiyo mwenyewe hasa
akiamini katika nguvu ya Mungu.
"Napenda
kuwashukuru wananchi waliofika hapa kwa kunitia
nguvu na pia kuwashukuru
madereva bodaboda akiwemo kijana Ahmed
kwa kujitolea mafuta ya petroli kwa ajili ya kukichoma chungu hiki "
Mbali ya
mzazi huyo kujitolea kuchoma chungu hicho na kuteketeza vitu vilivyokuwemo
ndani, wananchi waliofika kushuhudia tukio
hilo walilazimika kutimua mbio wakihofia zoezi hilo la uchomaji wa chugu.
(Picha/Habari
Na:-matukiodaima.com.





No comments:
Post a Comment