ELIMU:-Tarafa ya Murusagamba yapata Kinyago baada ya kupata chini ya wastani wa asilimia 52 katika Matokeo makubwa Sasa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 08, 2014

ELIMU:-Tarafa ya Murusagamba yapata Kinyago baada ya kupata chini ya wastani wa asilimia 52 katika Matokeo makubwa Sasa.

Tarafa ya Murusagamba haikufanya vizuri katika matokeo ya Darasa la saba mwaka jana (2013) kwa kuwa ya mwisho kati ya Tarafa 4 za wilaya ya Ngara mkoani kagera kwa kupata wastani wa chini wa 52% hivyo kuzawadiwa zawadi ya Kinyago kama ishara ya kufanya vibaya kitaaluma.


Zawadi ya kinyago kikinyanyuliwa na Mwakilishi wa tarafa ya Murusagamba ambayo imetoa pia Kata na shule ya mwisho kiwilaya na mkoa kwa kupata wastani wa chini katika mpango wa matokeo makubwa sasa,hivyo Kinyago walichozawadiwa ni kielelezo tosha kwa tarafa hiyo ya Murusagamba kuweka mikakati ya kukiondoa mikononi na kuwapa tarafa nyingine kwa kukazana Wadau,Walimu,Wazazi,Walezi na wanafunzi kushirikiana ili kuleta matokeo mazuri.


Shule ya Msingi Ntanga imekuwa ya mwisho kati ya shule 113 za wilaya ya Ngara kwa kupata wastani wa 16% huku pia ikiwa ya mwisho kati ya shule 903 za msingi kwa mkoa wa Kagera.




Baadhi la walimu walio tunukiwa vyeti kwa ajili ya ufundishaji wao uliofanya wilaya pamoja na wanafunzi kufaulu masomo yao.


Mkuu wa shule ya Sekondari Ngara,Mwl.Baraka akipokea cheti na zawadi  katika sherehe za wiki ya elimu   wilayani Ngara mkoani kagera.



Baadhi la walimu walio tunukiwa vyeti kwa ajili ya ufundishaji wao uliofanya wilaya pamoja na wanafunzi kufaulu masomo yao.


Katibu tawala wilaya ya Ngara,Bw.Vedastus Tibaijuka ambae alikuwa mgeni rasimi wakati wa  sherehe za wiki ya elimu   wilayani Ngara mkoani Kagera,  Pamoja na kutathimini mafaniko ya elimu na changamoto zake aliwataka wazazi,walezi  kuongeza ushirikiano kwa Walimu sambamba na Walimu kuzingatia Maadili ya kazi ili kuleta mafanikio katika elimu na matokeo makubwa sasa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya na Diwani wa kata ya Kibimba,Bw.John Shimilimana katika pozi wakati wa  sherehe za wiki ya elimu   wilayani Ngara mkoani kagera.

Afisa Elimu Sekondari wilaya Bw.Julius Nestory katika pozi wakati wa  sherehe za wiki ya elimu   wilayani Ngara mkoani kagera ambapo alibainisha kuwa jumla ya shilingi Milioni 157.9 zimepelekwa katika shule za bweni kwa ajili ya matumizi ya chakula ili kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi  huku kiasi cha shilingi milioni 450 kikitumika katika ujenzi wa maabara,matundu ya vyoo,matanki ya maji na nyumba za walimu katika idara ya sekondari.


Afisa Elimu shule za Msingi wilaya Bw.Saimon Mumbee katika pozi wakati wa  sherehe za wiki ya elimu   wilayani Ngara mkoani kagera

Baadhi la walimu walio tunukiwa vyeti kwa ajili ya ufundishaji wao uliofanya wilaya pamoja na wanafunzi kufaulu masomo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad