PICHA:-Taswira ya Ngara Volleyball ikiifunga Ingo Nawe ya Giteranyi-Burundi Seti 3-2 huku Walimu FC wakitoka sare ya 2-2 katika Soka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 16, 2014

PICHA:-Taswira ya Ngara Volleyball ikiifunga Ingo Nawe ya Giteranyi-Burundi Seti 3-2 huku Walimu FC wakitoka sare ya 2-2 katika Soka.

Timu ya mchezo wa wavu ya  Ingo Nawe ya Giteranyi-Burundi kushoto ikisalimia na timu Kombaini ya Ngara kabla ya kuanza mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa wa mchezo wa Wavu ambapo Ngara walishinda Seti 3-2,mchezo ukichezwa April 12, 2014,katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara.

Timu ya Kombaini Ngara katika picha ya Pamoja katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara.
Timu ya Ingo Nawe ya Giteranyi nchini Burundi  katika picha ya pamoja katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara.
Mgeni rasimi picha kushoto Katibu Tawala wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw.Vedastus Tibaijuka akifungua mchezo huo wa Wavu wa kirafiki wa kimataifa kati ya Kombaini Ngara dhidi ya Ingo Nawe ya Giteranyi-Burundi ambapo Ngara ilishinda kwa Seti 3-2.
Katika mchezo wa Wavu,timu ya Kombaini Ngara iliishinda Ingo Nawe ya Giteranyi-Burundi Seti 3-2-kwa Ngara kushinda pointi 25-15,27-25 na 15-7 huku Ingo Nawe ikishinda kwa 25-22 na 25-20,mchezo ukichezwa April 12, 2014,katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara.
Kutoka kushoto ni Afisa Michezo wilaya ya Ngara Said Salumu na Mgeni rasimi Katibu Tawala Vedastus Tibaijuka wakiteta jambo wakati mchezo ukiendelea ,katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara.
Picha juu na chini ni Mashabiki wakifatilia mchezo huo wa Wavu ambapo Ngara ilishinda pointi 25-15,27-25 na 15-7 huku Ingo Nawe ikishinda kwa 25-22 na 25-20,mchezo ukichezwa April 12, 2014,katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara.
Hapa mchezo umemalizika na wageni Ingo Nawe ya Giteranyi-Burundi ikifungwa Seti 3-2 na  Ngara.
Kikosi cha Timu ya soka ya Walimu FC kikiwa katika Picha ya Pamoja kabla ya kuvaana na wageni wao kutoka wilaya ya Giteranyi nchini Burundi ,timu ya Ingo Nawe ambapo katika mchezo huo wa April 12, 2014,katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara timu hizo zilifungana bao 2-2.
Kikosi cha  Ingo Nawe kutoka wilaya ya Giteranyi nchini Burundi kabla ya kuwavaa Walimu FC,katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara.
Mwamuzi wa mchezo huo wa  April 12, 2014,katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara.
Mgeni rasimi Katibu Tawala wilaya ya Ngara,mkoani Kagera Vedastus Tibaijuka alikuwepo kufatilia mchezo huo wa soka katika viwanja vya Kokoto mjini Ngara ambapo Walimu FC walitoka sare ya 2-2 na Ingo Nawe.
Kaimu katibu mkuu wa chama cha soka wilaya ya Ngara NDFA Bahati Kunzi mwenye shati la damu ya mzee alikuwepo kufatilia mchezo huo wa soka.
Muonekano wa uwanja wa Kokoto ambao ni uwanja wa soka wa wilaya ya Ngara,mkoani Kagera -ukiwa umejaa kokoto za mawe hali inayowafanya wachezaji kutocheza kwa raha kwa kuhofia kuumia.
Mashabiki na wapenzi wa soka kutoka wilaya ya Giteranyi na Ngara maeneo mbalimbali ya Ngara wakifatilia mchezo huo kati ya  Walimu FC walitoka sare ya 2-2 na Ingo Nawe.
....................Benchi la Ufundi la timu ya Walimu FC...............
....................Benchi la Ufundi la timu ya Ingo Nawe FC...............

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad