Matumaini ya
Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, yameanza kufifia baada
ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Sunderland Uwanja wa
Etihad jana April 16,2014 usiku.
|
MAN CITY
wamepata pigo kubwa katika mbio zao za Ubingwa baada ya kutoka Sare ya 2-2
kwenye Mechi ya Ligi Kuu Uingereza waliyocheza kwao Etihad na Timu ya mkiani
Sunderland.
Man City
walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya Pili tu baada ya Alvaro Negredo kuunasa
Mpira na kumpasia Sergio Aguero ambae alimsogezea Fernandinho, aliekuwa
akiingia ndani ya Boksi, na kupiga shuti la chini na kutinga wavuni.
Lakini
Sunderland walicharuka Kipindi cha Pili na Connor Wickham kupiga Bao 2 na
kuwafanya waongoze 2-1.
Ilibidi
Shuti kali la Samir Nasri liwaokoe Man City zikiwa zimebaki Dakika 2 na
kuifanya Mechi iwe Sare ya Bao 2-2 hadi mwisho.
Matokeo haya
yamewaacha Man City wakiwa Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 71 na sasa ndoto ya
Ubingwa kwao haiko tena mikononi mwao wenyewe.
Kwa Palace,
haya ni matokeo ambayo yamehakikisha usalama wao kubaki Ligi Kuu England.
Aidha Ile
azma ya Everton ya kumaliza ikiwa 4 Bora imeingia dosari kubwa baada ya
kufungwa wakiwa kwao Goodison Park Bao 3-2 na Crystal Palace.
Matokeo haya
yamewabakisha Everton nafasi ya 5 nyuma ya Arsenal
Position | Team | Played | Goal Difference | Points |
---|---|---|---|---|
1 | Liverpool | 34 | 51 | 77 |
2 | Chelsea | 34 | 42 | 75 |
3 | Man City | 33 | 54 | 71 |
4 | Arsenal | 34 | 18 | 67 |
5 | Everton | 34 | 21 | 66 |
6 | Tottenham | 34 | 0 | 60 |
7 | Man Utd | 33 | 18 | 57 |
8 | Southampton | 34 | 5 | 48 |
9 | Newcastle | 34 | -14 | 46 |
10 | Stoke | 34 | -10 | 43 |
11 | Crystal Palace | 34 | -14 | 40 |
12 | West Ham | 34 | -9 | 37 |
13 | Hull | 33 | -6 | 36 |
14 | Aston Villa | 33 | -14 | 34 |
15 | Swansea | 34 | -5 | 33 |
16 | West Brom | 33 | -11 | 33 |
17 | Norwich | 34 | -27 | 32 |
18 | Fulham | 34 | -40 | 30 |
19 | Cardiff | 34 | -34 | 29 |
20 | Sunderland | 33 | -25 | 26 |
No comments:
Post a Comment