![]() |
Kiongozi wa kwaya iliyotumbuiza katika hafla
hiyo akiimba atika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St.
Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo
Barani Afrika kwa mwaka 2013 .
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la
kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima hiyo
itatolewa jioni ya kesho, Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe
iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni
pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, ambaye
tayari amewasili mjini Washington kwa sherehe hiyo kubwa.
Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao
hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa watu wao
na limetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na
wenye mafanikio makubwa kwa masuala ya utawala bora.
Jarida hilo linasema kuwa ukweli wa hali hiyo bora ya utawala bora
chini ya uongozi wa Rais Kikwete umeendelea kumiminiwa
sifa kimataifa na leo umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kuigwa mfano kama
kituo cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa
katika sera na mifumo ya uchumi.
Jarida hilo
linasema kuwa Rais Kikwete alikuwa chaguo kubwa na la kwanza la
wasomaji wa Jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia mbali mbali za
mawasiliano za jarida hilo.
Linasema Jarida hilo, “Kuhusu maoni ya wasomaji wetu juu ya kiongozi
yupi wa Afrika ambaye ni hodari zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi na
maendeleo, matokeo ya majibu ya swali hilo yamedhihirisha bila shaka yoyote
kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika uongozi wa nchi yake. Na ushahidi uko
kila mahali – ameweza kusimamia uchumi ambao umekuwa kwa wastani wa asili mia saba kwa miaka yote ya uongozi
wake.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment